Picha ya pamoja na mgeni Rasmi.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewataka wanasheria kuwasaidia wananchi
kujua elimu ya sheria kutokana na wengi wao kushindwa kujua sheria hali ambayo
inasababisha wengi kukosa haki zao za msingi pindi wanapofuatilia haki zao.
Hayo ameyasema
wakati akifungua taasisi isiyo ya kiserikali ya msaada wa kisheria ya Himiza
Social Justice Wilayani humo, amesema
elimu ya sheria na ushauri ni muhimu sana na kwamba kesi za migogoro ya
ardhi mirathi, kesi za jinai na madai ni
nyingi kutokana na wengi kutokujua kesi hizo wanaweza kuzipeleka sehemu gani
kwa ajili ya msaada.
Na kwamba
watu wengi ambao wamekuwa wakikwama kesi zao wamekuwa wakikimbilia kwenye ofisi
ya mkuu wa Wilaya jambo ambalo ni ngumu kwa Mkuu wa Wilaya kuingilia kwani Mahakama
ni chombo huru kisichoingiliwa na muhimili wowote ule .
“Mahakama ni
muhimili ulio huru kumejengeka desturi ya baadhi ya wananchi Wilayani hapa kuja
ofisini kwangu kuomba msaada wa kisheria jambo ambalo sio sahihi natoa Wito kwa
wananchi kutambua kuwa huwezi kuingilia muhimili huu ni vyema wakawaoana
wanasheria na mahakimu kwa msaada zaidi”Alisema Kapufi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Bernad Otieno,ameelezea kuwa kuanzishwa kwa
taasisi hiyo ni kutokana na kuwepo
kwa tatizo la msaada wa kisheria hususani kwa watu wasiojiweza ikiwa ni pamoja
na upungufu wa mawakili kwa maeneo ya vijijini.
“Vijana
wachache Nikiwemo Mimi ,waliamua kuanzisha shirika hili walitamani na
wanatamani kuongeza ubora wa upatikanaji wa haki katika jamii kupitia utoaji wa
msaada wa kisheria ,ujenzi wa uwezo kwenye mambo ya kisheria na haki za
biashara”Alisema Otieno.
Otieno
aliongeza kuwa hadi Mwaka jana Tanzania Ilikuwa na sheria ya upande mmoja ya
utoaji wa msaada wa kisheria iliyokuwa inajulikana kama The legal Aid(Criminal
Proceesings)Act Cap.21(Kabla haijafutwa) ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa
ikisaidia utoaji wa msaada wa kisheria kwa kiasi kikubwa kwa watu wenye makosa
ya mauaji ,sheria ambayo inatoa nafasi kwa watu wengine wanaoshitakiwa kwa
makosa ya jinai kupata msaada wa kisheria.
“Huu ndiyo
ulikuwa msukumo Mkubwa wa kuhakikisha jamii kubwa ya watu wa Geita na Tanzania Kwa
ujumla hawawezi kumudu gharama za uwakilishi mahakamani na hata za kumuajiri
wakili kwa shunghuli zao za kisheria”Aliongezea Otieno.
Hata hivyo
baadhi ya wananchi Wilayani Humo,Eva Alex na Getruda Alias wamesema kufunguliwa
kwa ofisi hiyo itatoa msaada mkubwa wa kisheria kwani ni muda mrefu wananchi
wamekuwa wakikosa haki zao za msingi kutokana na kutokujua sheria hivyo ofisi
hiyo itakuwa mwarobaini wa matatizo ya kisheria.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: