MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKANUSHA TAARIFA ZA KUZUHILIWA KUINGIA MGODI WA BULYANHULU

Share it:
Image result for Mkuu wa Mkoa wa shinyanga





Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amekanusha taarifa zinazosambaa kwa kasi mtandaoni kuwa amezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Maduka Online imemtafuta kwa njia ya Simu kutaka kujua taarifa hizi kwa undani zaidi kama zinaukweli ndani yake ambapo amekanusha kuwa akuna ukweli bali ni maneno ya baadhi ya watu ambao awajui hali ilivyoendelea

“Ilikuwa ni ziara ya Kushtukiza kwa sababu kule mgodini wanatoka watu wa TMAA ambao wanakaa kule mgodini kwa niaba ya serikali ambao wanatakiwa wahojiwe,kwa hiyo watu wote wakatakiwa waondolewe mgodini,migodi sasa ikabaki haina uwakilishi wa serikali”,

“Kama mkoa tukasema kama hakuna mwakilishi wa serikali maana yake ni zamu yetu kuweka lindo la kwetu,lazima tukahakikishe kwamba migodi hiyo iko salama kwa maana ya kile kinachozalishwa kwani migodi inaweza kutumia mwanya huo kusafirisha dhahabu ambayo wameshaitengeneza”.

“Pamoja na kwamba tuliweka walinzi jana,tumeona ni vyema tukaangalie ambacho kipo hasa kilichozalishwa ni nini,kwa hiyo tukaanza na mgodi wa Buzwagi,tukaona dhahabu iliyozalishwa,wakatupeleka kwenye Chumba maalum cha dhahabu yaani "gold room",tukakuta mabaa za dhahabu tukahesabu,tukayapima kujua yapo kiasi gani,tukawaambia kwa kuwa watu wa TMAA hawapo,wasitengenezee baa zingine mpaka pale serikali itakapoleta hao watu kwani hao ndiyo wanahakiki kile kinachozaliwashwa”,-Telack.



“Baada ya kutoka Buzwagi tukaenda Bulyanhulu,tumeingia vizuri mgodini mpaka kwenye gold room,tulipofika sasa tukashindwa kuingia mahali ambapo dhahabu inahifadhiwa,sababu waliyotoa ni kwamba walifungua asubuhi na wao wakishafunga wanaset na muda kuwa kesho watafungua saa ngapi,kwa hiyo haiwezi kufunguka mpaka kesho,tulichokifanya tumeacha ulinzi wa kutosha pale ili kuhakikisha kuwa dhahabu ambayo tayari imezalishwaa isiweze kusafirishwa kinyemela kwani watu wa TMAA hawapo,kwa hiyo tutarudi kesho ili kujua kiasi gani cha dhahabu kipo”-RC Telack.



TAARIFA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

Habari za jioni, taarifa zinazosambaa kuwa Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amezuiwa kuingia mgodini Bulyanhulu. Taarifa hizo si za kweli. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu leo kujionea shughuli za uzalishaji bila kuwepo maafisa wa TMAA. Baada ya kuona uzalishaji ameagiza uyeyushaji wa dhahabu "melting" usiendelee bila kuwepo maafisa hao.

 Katika mgodi wa Bulyanhulu,mhe. Mkuu wa Mkoa ameagiza jeshi la Polisi kulinda Chumba maalum cha dhahabu yaani "gold room" kutokana na kushindikana kufunguliwa kwa madai kuwa kimefungwa kwa program maalum ya masaa 24.

 Hivyo jeshi la Polisi linalinda eneo hilo hadi hapo kesho saa 12.00 asubuhi chumba hicho kitapofunguliwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa atashuhudia.

Afisa Habari,

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Shinyanga.

25/05/2017.
Share it:

Post A Comment: