Wachimbaji wadogo wanne wamekufa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo madogo ya nyamalimbe yaliyopo wilayani Geita mkoani hapa.
Watu saba walifukiwa ambapo kati yao watatu wameokolewa na wamelazwa katika Kituo cha Afya Katoro.
Tukio hilo limetokea saa mbili asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Geita ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya Herman Kapufi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Waliofariki kwenye Tukio hilo ni Robart Kazelemwa (29) Msukuma Mkazi wa Kaduda Kata ya Katoto,JeremiaEmmanuel (29)Msukuma Mkazi wa Ushirombo ,Makena Mwita (29)Mkurya Mkazi wa Serengeti na Julius Timotheo(20)Msukuma Mkazi wa Katoro
Maiti zote zimetolewa na Taratibu za kusafirisha zinaendelea.
Post A Comment: