Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kido akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Mjini D |
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na washiriki wa mafunzo (hawapo pichani) yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ( hayupo Pichani) yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na washirki wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
24/05/2017
Redio za jamii nchini zimeshauriwa kutotumiwa na wanasiasa katika uendeshaji wa kazi zao bali zizingatie dhumuni kuu la kuelimisha wanajamii katika kuleta maendeleo ya Jamii.
Hayo yamesemwa na leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe, Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini kwa waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Mhe. Anstazia Wambura amesema kuwa Redio za Jamii zinatakiwa kusimamia malengo yao makuu ya kuwa karibu na jamii husika na kuzifanya jamii hizo kunufaika na Redio hizo na sio kufarakanisha jamii.
“ Nisistizie kwa washiriki kuzingatia malengo ya mafunzo haya mnayopewa ili yasaidie katika kuielimisha jamii katika masuala mbalimb ali na kuachana na masuala ya siasa” Alisistiza Mhe. Anastazia.
Mhe. Anastazia Wambura amesisitiza kuwa wataalamu wa habari wanatakiwa kutumiwa vizuri katika Halmasahuri nchini ili kuzisaidia Redio za Jamii ziweze kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.
Waandishi wa habari kutoka katika Redio za jamii nchini pamoja na wawakilishi kutoka Hamlashauri za Wilaya nchini wapo katoika mafunzo ya siku mbili yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini yanayofanyika Mjini Dodoma.
Post A Comment: