Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Richard Jordinson Akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga vifaa vya ujenzi. |
Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Richard Jordinson |
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl ,Herman Kapufi akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kwaajili ya ukaguzi wa vifaa ambavyo vimetolewa na GGM. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mkuu wa Wilaya Hiyo wakikagua vitu ambavyo vimetolewa na Mgodi. |
Mkuu wa Magareza Wilayani Geita,Mrakibu Mwandamizi Elly Maiga akishukuru kwa msaada ambao umetolewa. |
Mgodi wa
dhahabu wa Geita GGM Uliopo Mkoani Geita umefadhili vifaa vya ukarabati wa
bomba la maji taka Kwenye Gereza la Wilaya Hiyo vyenya thamani ya Sh Milioni
Sabini (70).
Akikabidhi
vifaa hivyo Mkurugenzi wa Mgodi huo ,Richard
Jordinson amesema kuwa jumla ya sh milioni sabini zimeweza kugharamia
kununua vifaa na kwamba walipokea maombi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na mkuu wa
Wilaya
wakihitaji Mgodi kufadhili vifaa hivyo.
“Tulipokea
maombi ya kuombwa kusaidia vifaa vya ujenzi kwenye Gereza la wilaya kutokana na
kwamba sisi pia ni jamii na siku sote tunapenda kuona jamii inayotunzunguka
inanufaika na uwepo wetu”Alisema Jordinson.
Akipokea
vifaa hivyo na kuvikabidhi kwa mkuu wa Gereza Wilaya ya Geita,Mkuu wa Mkoa Meja
jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga ameushukuru mgodi huo huku akisisitiza ujenzi
kufanyika kwa weledi zaidi.
“Tunawashukuru
wenzetu wa Geita Gold Mine kwa ushirikiano wao ambao wametuonesha ujenzi
ufanyike kwa weledi vile vile thamini ya msaada ambao umetolewa uonekane ili
hali ya magereza iwe nzuri pia tuepukane na magonjwa haya ya mlipuko”Alisema
Kyunga.
Aidha kwa
upande wake Mkuu wa Magareza Wilayani Geita,Mrakibu Mwandamizi Elly
Maiga,amesema kuwa baada ya mradi huo kuwa umekamilika utasaidia kuondokana na
hali ya magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu na maji taka ambayo yalikuwa
yakitoa harufu kali kwenye Eneo hilo.
Pia ameendelea kuwaomba wadau wengine kuguswa na kuendelea kuchangia huduma mbali
mbali za magerezani kwani changamoto bado ni nyingi.
Gereza la
Wilaya ya Geita lilianza mnamo mwaka 1947 wakati huo lilikuwa na uwezo wa
kuhifadhi waalifu arobaini na Moja
kadili siku zinavyozidi kwenda linazidi kuwa dogo kwani watu wamekuwa
wakifikia idadi ya mia tano hadi mia sita kwa sasa.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: