MKURUGENZI WA MJI WA GEITA ATANGAZA KIAMA KWA WAFUGAJI WAOINGIZA MIFUGO MJINI NA KWENYE VYANZO VYA MAJI

Share it:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinal akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo Kiwilaya yamefanyika Kwenye Halmashauri ya Mji huo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Geita,Janeth Mobe akisoma Hotuba kwa niaba ya Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Mazingira.
Afisa Mazingira ya Halmashauri ya Mji wa Geita Packrasi Shokelela akielezea mikakati ya utunzaji wa Mazingira kwenye Halmashauri Hiyo.

Wananchi ambao wameuzulia kwenye maadhimisho ya Wiki ya Mazingira.

Msanii wa Mashairi akiimba shairi la Mazingira.

Afisa Mazingira Geita Mji Melkizedeck Alfred Mushi akisoma Risala Mbele ya Mgeni Rasmi.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwatulole Wakipongezwa na Mgeni Rasmi Kutokana na kufanya vizuri kwenye swala la utunzaji wa Mazingira.


Wanafunzi wakifuatilia kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwenye maadhimisho ya Wiki ya Mazingira.
Wakati watanzania wakiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita  Mhandisi Modest Aporinali amewaonya wafugaji kutoingiza mifugo yao katikati ya mji na kwenye vyanzo vya maji.

Hayo ameyasema wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira ambapo Kiwilaya wameadhimisha kwenye Halmashauri ya Mji,amesema kuwa kumekuwa na desturi ya wafugaji kuachia mifugo kwa kisingizio cha shida ya maji na mingine kuingia katikati ya mji bila ya watu kujua kuwa maeneo ya mjini mifugo haitakiwi na kwamba wataanza msako wa kukamata mifugo ambayo itaonekana ikizagaa.

“Leo tunaadhimisha siku ya Mazingira Duniani lakini kuna swala ambalo linanisikitisha sana kwa mifugo kuingia mjini na kuharibu vyanzo vyetu  vya maji na hili mkuu wa Wilaya ninaomba tuliangalie sana kwa umakini maana haiwezekani kuendelea kuharibu maeneo ya mjini kwa sababu ya wingi wa mifugo katikati ya mji”Alisema Modest.

Akimwakilisha   Mkuu wa Wilaya ya Geita Ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi Kwenye Maadhimisho hayo,Bi Janeth Mobe  amewataaka wananchi kutambua kuwa halmashauri ya mji ni tofauti na ya vijijini na kwamba jambo ambalo amelisema mkurugenzi watahakikisha wanaliunga mkono  na msako wa kukamata mifugo itakayoonekana hovyo mjini inakamatwa .

“Jamani nawaomba wananchi Mtambue kuwa tupo halmashauri ya Mji sio vijijini sasa swala la mifugo mjini hatuwezi kukubaliana nalo na ninamuunga mkono Mkurugenzi Juu ya agizo hili na nitahakikisha Mkuu wa Wilaya linamfikia hili swala haraka iwezekanavyo ili kuondoa mifugo kwenye mji wetu wa Geita inatakiwa kuwa kila mtu awe mtunzaji wa Mazingira yetu”Alisisitiza Mobe.

Kwa upande wake afisa usafishaji na Mazingira kwenye Halmashauri Hiyo bw Packrasi Shokelela amewataka wafugaji kujibu mifugo ambayo inakubalika kwa mjini na kwamba kwa sasa sheria itaanza kufanya kazi kwa yeyote ambaye atakuwa yupo kinyume na makubaliano ya sheria za mifugo kwa upande wa mjini.

“Nataka kuwaambia tu kwamba swala la mifugo mjini halitakiwi na tunasisitiza kama kuna mtu au watu wanafuga mifugo mjini wachukue hatua ya kurudisha mifugo hiyo vijijini ambako kuna maeneo makubwa ya kufugia kwani mjini kumebanana”Alifafanua Shokelela

Wiki ya mazingira imefanyika Kitaifa Mkoani Mara Wilaya ya Butiama Huku kauli mbiu ikiwa ni ,” MAHUSIANO ENDELEVU KATI  YA BINADAMU NA MAZINGIRA”

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.


Share it:

habari

Post A Comment: