|
Baadhi ya wazazi,walimu na Wanafunzi ambao wamehudhulia kwenye maadhimisho ya wiki ya Elimu. |
|
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita na Diwani wa Kata ya Buhalahala ,Musa Kabesse akielezea mikakati ya kielimu. |
|
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Nyamalembo wakicheza ngoma ya utamaduni kutoka Mkoa wa Kagera. |
|
Diwani wa Kata ya Nyankumbu Michael Kayapa akijitambulisha wakati wa shughuli ya maadhimisho ya wiki ya Elimu. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Majagi Majagi alisema halmashauri ya mji itaendelea kutoa sapoti ya kutosha. |
|
Kaimu afisa Elimu Msingi Halmashauri ya mji Bi ,Khadija Ubuguyu akisoma taarifa ya Elimu kwa Halmashauri hiyo. |
|
Wanafunzi wa shule ya Msingi WAJA Wakiimba wimbo mbele ya mgeni Rasmi. |
|
Mwalimu Mkuu wa Umahiri wa shule ya Msingi Kalangalala Rachel Jumanne Akimuonesha Mgeni Rasmi Shughuli ambazo wanazifanya na wanafunzi. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiangalia kwa umakini namna ambavyo mwanafunzi ambaye anatokea kwenye Kituo cha Elimu ya watoto wenye ulemavu. |
|
Elysalver Nkanga mwakilishi wa afisa Elimu Mkoa wa Geita akitoa neno la kuwashukuru walimu na wazazi kwa jitihada ambazo wameendelea kuzitoa kwenye sekta ya Elimu Mkoani humo. |
|
Katibu wa chama cha Walimu Wilayani Geita,John Kafimbi akielezea mikakati ya chama katika kuendelea kuinua Elimu . |
|
Mkuu wa Wilaya akimkabidhi cheti cha Kufanya vizuri na kushika nafasi nzuri ya kielemu Mkuu wa shule ya Msingi WAJA. |
Wananchi
Katika Wilaya ya Geita wametakiwa kuwafichua watu ambao wameendelea na vitendo
vya ulawiti dhidi ya watoto ambavyo
vinaendelea kufanywa na Baadhi ya watu watu wasio na mapenzi mema kwa watoto.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl Herman Kapufi wakati wa kufunga Wiki ya Elimu kwenye
Halmashauri ya Mji wa Geita amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikichukua
nafasi kubwa sana na watoto ambao wanalawitiwa ni watoto wale wa kuanzia miaka
8 hadi 13 ambapo wanakuwa bado hawajajitambua.
Ameongeza
kuwa maeneo ambayo yanaongoza kwa
vitendo hivyo ni maeneo ya Miji Mikuu Kasamwa,Bukoli,Mgusu ,Nyarugusu ,Mgusu
,Lwamgasa na Geita Mjini ni maeneo ambayo yanaonekana kuwa na vitendo hivi kwa
watoto na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na kuwafichua
wale wote ambao wanafanya Tabia hizo.
“Inasikitisha
sana kuona vitendo vya ukandamizaji vinaendelea kwa watoto wadogo ambao hawana
hatia jamii haitakiwi kuendelea kuvifumbia macho vitendo vya namna hii na watu
ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivi wengi wao ni wale ambao unamkuta baba
anamuoa mama anamkuta na watoto wale watoto anakuwa hawapendi mwisho wa siku
anajikuta akiwalawiti na maeneo ambayo
vitendo hivi vimeshamiri kwenye Wilaya yangu ni maeneo ambayo yanamzunguko wa
Biashara ,kama Kasamwa,Katoro,Mgusu,Nkome,Nyarugusu ,Lwamgasa na Geita mjini
hivi vitendo vimeshamiri sana kwa maeneo hayo”Alisema Kapufi.
Kaimu afisa
Elimu Msingi Halmashauri ya mji Bi
,Khadija Ubuguyu ameelezea mikakati ya kuinua elimu idara za msingi na
sekondari kuwa ni ufuatiliaji wa Taaluma mashuleni ili kuhakikisha wanaendelea
kubaki kwenye nafasi nzuri kitaaluma.
“Kuendelea
kufanya mitihani ya majaribio,kuunda makundi ya ujirani kwa watoto waishio
karibu ili waweze kujisomea muda wa jioni baada ya masomo ya darasani na
kushirikisha jamii kupitia kamati na bodi za shule kufuatilia taaluma mashuleni,nidhamu
walimu na wanafunzi pamoja na kudhibiti utoro mashuleni kwa walimu na wanafunzi
“Alisema Ubuguyu.
Aidha kwa
upande wake Kaimu Afisa Elimu Mkoa humo,Elysalver Nkanga amesema kuwa mafanikio ambayo yamepatikana ya
kielimu yanatokana na mshikamano Baina ya Walimu na wanafunzi na kuwa na kauli
moja ambayo imeendelea kuwajenga vijana kuwa juu kwenye masomo yao.
Juma la wiki
ya Elimu limeambatana na kauli mbiu isemayo” ELIMU BILA MALIPO HAINA MAANA NI
BURE JAMII INA NAFASI YA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU”Lengo likiwa ni
kuwakumbusha wananchi jukumu la kuwekaza kwenye Elimu kwa kushirikiana na Serikali
kwa kujitoa kwa hali na mali.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: