Yanga imetupwa nje ya michuano ya Kombe la SportsPesa Super Cup. Sasa inaifuata Simba kupumzika "nyumbani" baada ya juzi nayo kutolewa kwa Nakuru All Stars kwa mikwaju 5-4 ya penalti.
Katika mechi hiyo ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga imetupwa nje baada ya kuchapwa na AFC Leopards kwa mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kwa suluhu.
Kiungo Said Juma Makapu na kinda Said Mussa ndiyo waliopoteza mikwaju ya penalti baada ya nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Obrey Chirwa kufunga.
Wakenya walionekana ni watulivu katika upigaji wa mikwaju ya penalti.
Maana yake sasa, bingwa wa michuano hiyo lazima atatokea nchini Kenya.
Post A Comment: