Mbunge Msukuma akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho.
PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLIE
Mbunge wa
Jimbo la Geita Vijijini Mh,Joseph Kasheku Msukuma ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita
ameongoza mamia ya wananchi wa kijiji cha Hiyanamilo Kata ya Nkome Wilayani
Geita kutoa visiki ambavyo viliwekwa na mtu ambaye inasadikika amenunua eneo la
kijiji linalokadiliwa kuwa ni hekari
moja na nusu ambalo lilitengwa kwa
matumizi ya stendi kutoka kwa serikali ya kijiji.
Hatua hiyo
imekuja baada ya Serikali ya Kijiji
ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ,Bw Thomas Alila na mtendaji wa kijiji
Charles Mbilingi kuuza eneo kwa kiasi cha sh ,Milioni sita (6).
Kwa maelezo
ya afisa mtendaji wa Kijiji Charles Mbilingi amesema kuwa tarehe 15 mwezi huu
walikaa kwenye kikao na wanakijiji na kuamua kwamba wauze eneo hilo ili liweze kusaidia ujenzi wa shule.
“Tulikaa
kama halmashauri ya Kijiji tukajadili namna ya kutatua changamoto ya kukosekana
kwa shule kwenye kijiji chetu tulipojadili tukaonelea kwa sababu tuna eneo ni
bora tuliuze ili tuweze kupata pesa ambazo zitasaidia ujenzi wa madarasa na
hatukufanya peke yetu
tuliwashirikisha wananchi wa kjiji wakawa
wamekubali”Alisema Mtendaji.
Hata Hivyo
kutokana na maelezo hayo ya mtendaji wa Kijiji Mbunge Msukuma amewaeleza wananchi ambao walikuwa
kwenye Mkutano wa hadhara kuwa eneo hilo liliuzwa tarehe tano mwezi huu jambo
ambalo yeye alilikataa kutokana na faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na
uwepo wa eneo hilo.
“Nimesikitishwa
sana na kitendo ambacho kimefanyika cha kuuzwa eneo hilo kiasi cha Shilingi
milioni sita (6) na mimi nilimpigia simu mtendaji nikamwambia azirudishe pesa aende halmashauri kuna
maelekezo kwa mkurugenzi na tutambue kuna maeneo muhimu lazima yawepo
leo(jana)ninakwenda kung’oa visiki vyote”Alisema Msukuma
Katika hali
isiyo ya kawaida Diwani wa Kata ya Nkome
Masumbuko Nsembe amejikuta jina lake likiwa limeandikwa kuwa ni miongoni kati
ya viongozi ambao walilidhia kuuzwa kwa
eneo la kijiji.
“Mheshimiwa
Mbunge mimi sikuuza nilifika saa kumi na moja nilikuta wakisoma hiyo taarifa ya
kuuza lakini mimi niliwaambia kuwa wasiuze eneo hilo kwa hicho kiasi.”Alisema
Diwani
Katika hali isiyo
ya kawaida wananchi ambao walihudhuria kikao
hicho cha kukubaliana kuuzwa kwa eneo hilo walipotajwa majina yao walijikuta wakidai
kushindwa kujua hali hiyo imetokana na nini na kama waliingizwa mkenge kwenye
mauziano hayo.
Kutokana na
hatua ambayo mbunge ameifanya ya kuongeza wananchi kutoa visiki wananchi
wameshukuru na kusema kuwa walikuwa hawajui
kama eneo lao limeuzwa.
|
Post A Comment: