Mkuu wa Mkoa wa Geita akioneshwa damu ambazo zilivuja baada ya marehemu kuwa ameanguka. |
Baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakitelemka kuelekea eneo ambalo vijana wamekuwa wakiingilia kwenye mgodi huo kwaaajili ya kutafuta mawe ya dhahabu (Magwangala). |
Eneo ambalo inasadikika vijana wamekuwa wakiingia kupitia maeneo ya juu. |
Sehemu ya shimo ambalo limekwisha kuchimbwa ambapo ni moja kati ya maeneo hatari ambayo wamekuwa wakiingia baadhi ya vijana kwaajili ya kutafuta mawe ya dhahabu. |
PICHA NA JOEL MADUKA.
Serikali ya Mkoani Geita imegharamia maziko ya kijana Shinje
Charles aliyefariki kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) huku ikitoa siku
saba (7) kuhakikisha upelelezi unafanyika kuhusu tukio hilo.
Mwili wa marehemu Shinje Charles umekaa kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita kwa siku kumi na moja (11) baada ya ndugu kugoma kuuzika wakishinikiza
uchunguzi wa kina wa tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
na kamati ya ulinzi na usalama kufika kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM kuangalia
maeneo yanakosadikiwa kuwa kijana huyo alianguka kwenye shimo liilokuwa
limechimbwa.
Hata hivyo baada ya kukutana na kuzungumza na uongozi wa
mgodi Mkuu wa Mkoa ,Amesema wao kama serikali wamechukua uwamuzi wa kuzika
mwili huo kutokana na kukaa muda mrefu
na kwamba swala la upelelezi wa kifo hicho wamemwachia kamanda wa Mkoa
kuhakikisha ndani ya siku saba (7) taarifa inapatikana.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Geita Bw Joseph
Msukuma amesema hatua ya serikali kuzika imekuja baada ya GGM kusema wako
tayari kutoa jeneza na gari na vitu vingine vichangiwe na wananchi.
“Kumekuwa na mvutano mkali GGM wanasema wako tayari kuchangia jeneza na gari
tulichokifanya namshukuru Mheshimiwa DC amesema wapeleke gari lao na jeneza
hivyo tulichokifanya dc ametoa lakini mbili na mimi kama mbunge nimetoa laki
sita ile gharama ya kwenda kumzika marehemu tayari anayo DC”Alisema Msukuma
Kaka wa Marehemu Bw James Charles amesema familia imekubaliana
na kauli ya Mkuu wa Mkoa ili mwili huo uzikwe wakati upelelezi ukiendelea
Makamu wa Rais wa mgodi wa GGM Bw Simon Shayo amesema huwa
wanachangia na sio kubeba gharama zote za msiba.
Kijana Shinje Charles alifariki August 21 mwaka huu baada ya
kuwa na wenzake walioingia nao mgodini kuchukua mawe ya dhahabu maarufu,
Magwangala .
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: