Mkaguzi wa bodi ya pamba wilayani maswa mkoani simiyu Ally Maborouk akiongoza operesheni ya kukagua pamba kwa kutumia mahakama inayotembea katika vituo mbalimbali vya kununulia pamba wilayani humo. |
Na COSTANTINE
MATHIAS, Maswa.
Bodi ya Pamba
Tanzania wilayani Maswa mkoani Simiyu imefanya operesheni maalumu ya kuwagakua
wanunuzi na wauzaji wa Pamba ambao wamekuwa wakichafua zao hilo kwa
kuichanganya mchanga, maji na udongo ili kuongeza uzito na kupata faida mara
mbili ambapo katika huku oporesheni wakulima na wanunuzi wamepongeza zoezi hilo
linaloondoa udanganyifu katika zao hilo.
Wakiongea katika
ukaguzi huo baadhi ya wanunuzi na wakulima katika vijiji vya Mwabayanda na Nguliguli
walisema kuwa zoezi hilo ni zuri kwa sababu linawafanya wajitathini na kufahamu
ubora wa pamba wanayoinunua pia kuwakumbusha wakulima kutoharibu pamba yao.
‘’zoezi hili
tunaomba liwe endelevu kwa sababu linagusa wakulima na wanunuzi kuwa yoyote
atakayekutwa na kosa anahukumiwa hapohapo, litaondoa uchafuzi wa pamba na
kuongeza ubora wake hivyo litakuza soko la pamba kimataifa ambayo awali ilikuwa
imeshuka kutokana na pamba yetu kuwa chafu’’ alisema Nkuba Minoja.
John Ng’hona
alisema kuwa pamoja na ukaguzi huo, katika msimu ujao watuletee mbegu ya pamba na pembejeo kwa wakati ili
tuweze kulima kwa uhakika na kuongeza uzalishaji.
Naye Mkaguzi wa Bodi
ya Pamba wilayani humo Ally Maborouk alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na
wanunuzi wanaoharibu pamba ni bora watafute biashara nyingine kwa kuwa bodi
hiyo inasimamia wauazaji na wanunuzi na kuhakikisha pamba inayozalishwa na
kuuzwa ni safi.
‘’wanunuzi
wanaoharibu pamba ni bora watafute biashara nyingine, tutahakikisha pamba yote
inayozalishwa na kuuzwa ni safi ili isiharibu soko la zao hilo kimataifa, tuko
imara tutahakikisha tunawashughilikia ipasavyo’’ alisema Maborouk.
Aidha katika zoezi
hilo lilioambata na mahakama inayotembea
(mobile court) imekagua vituo vya pamba katika vijiji vya Nguliguli,
Mwabayanda, Ilimbambasa, Senani, Zebeya na Mwabadimi na kuibua hoja baada ya
mnunuzi mmoja wa pamba kampuni ya Gaki kijiji cha Igumangobo kufunga kituo na kuwakimbia
wakaguzi hao.
Baada ya kuona
hali hiyo Mkaguzi wa Pamba aikifunga kituo hicho na kumwagiza mtendaji wa
kijiji kumkamata mnunuzi huyo ili aweze kueleza sababa zilizomfanya akikimbie
kituo chake.
Katika kijiji hichohicho cha
Igumangobo wanunuzi wawili Malugu Sungwandeba na George Salum wanunuizi wa
pamba Kampuni ya Kahama Cotton Co Ltd ya mjini Kahama mkoani Shinyanga
walipatikana na hatia baada ya kukiri kukutwa wamenunua pamba chafu
katika ghala lao
Katika mahakama hiyo inayotembea
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyalikungu,Lilian Kinyemi aliwahukumu washitakiwa
hao adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela kila mmoja au kulipa faini ya Sh
50,000 na Kampuni hiyo kuilipa bodi ya Pamba Sh 500,000 na washitakiwa walilipa
faini zote na kuachiwa huru.
Post A Comment: