Mchungaji,David Joseph Magige akiendelea na mahubiri kwenye Kanisa la EAGT Majengo mapya. |
Ikiwa kesho wananchi nchini Kenya wanatarajia kupiga kura ya
kumchagua Rais wa Nchi Hiyo ,Mchungaji wa Kanisa la EAGT Majengo mapya tawi la
Nyankumbu wilayani na Mkoani Geita David Joseph Magige amemtabiria ushindi mgombea wa Muungano wa
vyama vya siasa NASA ,Raila Odinga Kuwa rais wa Kenya.
Mchungaji Magige,katika mahubiri yake kwenye ibada ya Jana
Kanisani Hapo amesema utabiri wake unatokana na maono aliyofunguliwa na Mungu
katika sala na maombi yake.
“Ni mara ya tatu sasa Rohoo mtakatifu amekuwa akinifunulia
maono ingawa nimekuwa ni muoga sana kujitokeza na kutamka mbele za watu mara ya
kwanza ni uchanguzi Mkuu wa nchini kwetu nilioteshwa kuwa Rais ambaye atashinda
ni Magufuli lakini sikuweza kusema,na bado hata Marekani pia wakati wa mchakato
wa uchaguzi nilipata maono kuwa ambaye atakalia kiti cha urais ni Donald Trump
lakini pia nilisita kusema nilimwambia Mke wangu awamu hii nasema ni Raila Odinga
ndiye ambaye atashinda kiti cha Uraisi maana ni changuo la Mungu”Alisema
Mchungaji Magige.
Aidha, mchungaji Magige amewataka waumini wake pamoja na
Watanzania kwa ujumla kuendelea
kuliombea taifa la Kenya ambalo litafanya uchaguzi mkuu August 8 mwaka huu na
pia kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.
Uchaguzi huo unawahusisha wagombea urais wawili ambapo Rais
anayemaliza muda wake Uhuru Kenyata na Mgombea anayeungwa mkono na umoja wa
vyama vya upinzani NASA Bw. Raila Odinga.
Post A Comment: