Mwakilishi wa mgodi wa GGM Kwenye baraza Hilo
Bw Joseph Mangilima akitoa ufafanuzi juu ya madai ambayo yanadaiwa na Halmashauri.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Halmashauri ya mji wa Geita imeitaka kampuni ya madini ya dhahabu ya Geita (GGM) kulipa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni 11.045 ambazo ni madai ukwepaji wa kodi ya huduma kwa kipindi cha mwaka 2004 hadi 2013 nakuipa muda wa mwezi mmoja endapo itashindwa itaupeleka Mgodi Mahakamani.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Eng. Modest Apolinary,Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Constantine Morandi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola.
Mgodi wa GGM ulianza uzalishaji mwaka 2000 na kuingia makubaliano na Wizara ya nishati na madini ya kulipa dola 200,000 kwa halmashauri kila mwaka lakini inadaiwa haikulipa hadi mwaka 2004 kwa madai kuwa halmashauri haina sheria inayoelekeza walipwe kiasi hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amesema kuwa wametoa siku 30 fedha zilipwe na endapo hawatalipwa basi wataupeleka mgodi Mahakamani kwakuwa sheria zipo wazi inayowataka kulipa asilimia 0.03
Awali akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwanasheria wa Halmashauri ya mji Queen Luvanda amesema Madai hayo yanatokana na kodi ya huduma ambayo kampuni ilipaswa kulipa kwa mujibu wa sheria.
Mwaka 2004 Halmashauri ilitunga Sheria ndogo ya kodi ya huduma ya asilimia 0.03 ya mauzo ya mwaka na kuanzia sheria itungwe mgodi hawakulipa asilimia 0.03 bali walilipa dola laki mbili kuanzia mwaka 2004 hadi 2013 kinyume na maelekezo ya sheria inavyosema.
Maneja Kitengo cha Mahusiano katika Mgodi wa GGM Joseph Mangilima amesema sheria ya kodi ya huduma ilitungwa mwaka 2004 na ikaanza kufanya kazi mwaka 2005 na Kampuni ilikua ikilipa dola 200,000 kila mwaka kwa mujibu wa sheria
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
|
Post A Comment: