Wajumbe ambao ni madiwani wa halmashauri mbili ya Mji na Wilaya ya Geita pamoja na watumishi mbali mbali wakifuatilia kikao taarifa na maadhimio juu ya kikao ambacho kinaendelea. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama akielezea juu ya hatua hizo ambazo zimechukuliwa na mabaraza hayo. |
Mbunge wa Geita ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Joseph Kasheku Msukuma,akielezea na kuunga hoja ambayo imetolewa na wajumbe. |
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Geita ,Akisoma taarifa na maadhimio juu ya Mgodi wa GGM. |
Baraza maalum la madiwani lililojumuisha Madiwani wa
Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Geita limesema hawako tayari kushirikiana na
mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM hadi mgodi utakapokuwa tayari kuwalipa Dola 12,645,345.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa madai yatokanayo na
kodi ya huduma kutoka mgodi wa dhahabu wa GGM, madai ya kuanzia mwaka 2004 hadi
2013.
Hali hiyo imesababisha madiwani wa Halmashauri zote mbili
kukutana kwenye kikao ambacho kimewahusisha watendaji wa halmashauri zote,
wananchi na afisa kutoka mgodi wa GGM na kuutaka mgodi huo kusitisha huduma za
jamii ambazo walikuwa wakizifanya pamoja
na magari ya kampuni hiyo kutotumia barabara za Halmashauri hizo pamoja na
kuzuia huduma ya maji kufika kwenye mgodi huo.
Magulu Kuzenza ambaye ni diwani wa kata ya Bukondo, Elias
Ukumu Diwani wa Nyachiluluma na Bi Amina Swedi Kanijo wameeleza kuwa hawawezi
kuendelea kuubembeleza mgodi huo
Akisoma taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa ya wafanyabiashara
Kaimu Mwenyekiti wa TCCIA John Luhemeja ameelezea mapendekezo ya kamati hiyo
juu ya namna ambavyo wamewaza kubaini ujuma ambazo zinafanywa na mgodi huo.
“Tumefatilia tukabahini kuwa kuna ujuma ambazo zimeendelea
kufanywa na baadhi ya watendaji wa mgodi wa GGM kwa kushindwa kutoa fursa za
ajira kwa maeneo haya na mwisho wa siku kujikuta wanatoa ajira kwa watu wa kanda ya kasikazini ikiwemo swala la
tenda hivyo tunaamini tamko letu la leo litatoa mstakabari juu ya mambo ambayo
yanafanywa na mgodi”Alisema Luhemeja
Kutokana na mapendekezo ambayo yametolewa ya mgodi
kutokupitisha magari yake kwenye Halmashauri hizo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama
Wilayani Humo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amesema kuwa
hatawaandikia barua GGM wasipitishe magari kwaajili ya usalama na pia hatatoa
taarifa kwa mkuu wa mkoa juu ya mgogoro uliopo kwenye halmashauri hizo.
Kwa upanda wake Meneja mwandamizi wa mahusiano kwenye mgodi
huo Manase Ndoloma ,amesema kwa upande wao wanaheshimu mabaraza yote mawili na
kwamba kwa swala la hilo surusheni yake ni mahakamni na kwamba wapo tayari kwenda mahakamni kwani
ndio chombo pekee ambacho kinatoa haki .
Utekelezwaji wa agizo hilo unatarajia kuanza kesho muda wa
saa sita za usiku kwa kuzuhia magari kuingia kwenye halmashauri zote mbili na
bomba ambalo lipo Rungwe kufungwa.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: