Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Katika kuelekea ujenzi wa
Tanzania ya uchumi wa kati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John
Pombe Magufuli, Kiongozi anayesifika kwa uchapakazi, mtu wa watu, mtu
wa wanyonge na Mzalendo kwa kusimamia rasilimali za Taifa ambaye
ameonyesha nuru kubwa kwa watanzania.
Katika hotuba zake mbalimbali
amekuwa akisisitiza wananchi kufanya kazi na kuienzi kauli mbiu yake
“HAPAKAZI TU” huku katika utendaji kazi wake Rais Magufuli ameonesha
dira kubwa kwa kuanza na miradi mikubwa ambayo itaipeleka nchi katika
uchumi wa kati na wenye viwanda na huduma nzuri kwa jamii, watanzania
wanatakiwa kumuunga mkono ili aweze kuifanya kazi yake kwa ufasa kwa
kuanzisha, kuendeleza na kumalizia miradi ambayo ipo mikononi mwake.
Kama alivyoahidi wakati wa kampeni
kwamba Serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi huku akiwa mstari wa mbele
katika kuchapa kazi na alipewa jina la uchapakazi kama Tinga Tinga
yani mtu wa kazi, ni miradi mingi ambayo Serikali yake imefanya na
inaendelea kufanya mambo makubwa Kama yalivyoainishwa na mwandishi wa
makala hii.
- Barabara za Juu (Fly Over).
Aprili 16 ya mwaka 2016 uzinduzi
rasmi wa ujenzi wa barabara za juu ulifanyika Jijini Dar es Salaam
katika makutano ya barabara ya Tazara ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, barabara
ambayo itaondoa msongamano wa magari katika Jiji hilo na kuweza kusaidia
kuokoa upotevu wa mapato utokanaona watu kuchelewa kazini na kwenye
shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Faida kubwa ya barabara hii
itatupunguzia fedha zilizokuwa zikipotea, katika tafiti zilizofanywa
mwaka 2013 tulipoteza billion 411.3 katika Jiji la Dar es Salaam pekee
kwa sababu ya msongamano mkubwa”, alisema Rais Magufuli.
Mradi huu mkubwa ambao utagharimu
fedha za kitanzania shilingi billion 101.6 unafadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Japan (JAICA), ambapo Shirika hilo litatoa kiasi cha
shilingi billion 93.44 na Tanzania ikitoa billion 8.36,Mradi huu ambao
ni wa aina yake Tanzania unatarajia kumalizika ifikapo oktoba 2018, huku
barabara nyingine ya aina hiyo iliyoko makutano ya Ubungo ikitarajiwa
kamilika ifikapo 2020 na kuwezesha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
kufurahia maisha kwani sasa wataondokana na adha ya usafiri hivyo kuwahi
kwenye maeneo yao ya kazi kuchapa kazi na kuijenga Tanzania ya viwanda.
- Bomba la Mafuta Ghafi (Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanzania).
Ilikuwa ni siku ya pekee kwa
wananchi wa chongoleani ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseveni
walizindua mradi mkubwa ambao ni wa kipekee duniani.
Ni bomba ambalo lina urefu wa
kilomita 1445 huku Tanzania likichukua sehemu kubwa yaani kilomita 1115
na kilomita 130 ni kwa upande wa Uganda, ni mradi ambao utagharimu kiasi
cha dola za Kimarekani billion 3.5 na utasimamiwa na kampuni tatu yaani
SNOOC,TOTALE zote kutoka nchini Ufaransa pamoja na TUROL ya Uingereza
na unatarijia kukamilika mwaka 2020.
“Ni mradi wa kipekee duniani kwa
kuwa mradi kama huu upo India ambao unasafirisha mafuta ghafi lakini una
kilomita 600 tu, kwa hiyo bomba hili ni la kwanza duniani”, alisema
Rais Magufuli.
Mradi huu utapita katika Mikoa
nane kwa Tanzania bara Wilaya 24 huku Vijiji 184 vikifaidika na mradi
huo mkubwa wa kipekee ambao utatoa ajira 10,000 wakati wa ujenzi na
1,000 kwa uendeshaji wake, Wahenga walisema “Kizuri kula na nduguyo”
ndivyo ilivyo kwa Rais Museveni wa Uganda kukubali kushirikiana katika
mradi huu mkubwa kwa kupata ushawishi mkubwa wa usalama kutoka kwa Rais
mchapakazi Dkt.John Pombe Magufuli (Tinga Tinga).
- Kufufua Shirika la Ndege (Air Tanzania).
Serikali ya Awamu ya Tano
ilianzisha nia na matumaini katika kukuza na kuimarisha sekta ya
uchukuzi kwa kufufua shirika lake la ndege (ATCL) ambalo mwaka 2016
lilianza rasmi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kununua ndege zake
mpya ambazo zimekuwa zikisaidia Watanzania hususani wafanya biashara
waendao mikoani mara kwa mara kwa kupunguza gharama kubwa za usafiri.
“Tumeleta bombardier Q 400
imepunguza gharama za safari kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza wanalipa
160,000 hadi 200,000 wakati nauli ilikuwa imeshafikia hadi 800,000 kwa
safari za Dar es Salaam –Mwanza”, alisema Rais Magufuli.
Mnamo septemba 2016 serikali ya
awamu ya tano ilileta ndege mbili aina ya Bombadier Q400 ambazo
litengenezwa nchini Canada, katika matarajio yake inatarajia kuwa na
ndege 7 ambapo kwa awamu ya kwanza zimekuja mbili , lakini pia ndege
mbili aina ya Jeti CS 300 zenye uwezo wa kubeba abiria 137-150
zitaletwa nchini 2018 , bila kusahau ndege kubwa aina ya Boen 787-8
Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo nayo italetwa waka
2018, itasaidia kwa safari za kimataifa kwani itakuwa na uwezo wa kutoka
moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
hadi Marekani ama Ulaya bila kutua kokote.Huu ni mradi ambao utaleta
fursa ya maendeleo hususani katika sekta ya utalii.
- Sekta ya Utalii.
Sekta ambayo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ameendelea kuinua zaidi
ni Sekta ya Utalii baada ya ununuzi wa ndege ambazo zitakuwa kimbilio
katika kukuza na kuimarisha Utalii nchini.
“Huwezi kuendeleza nchi bila kuwa
na Watalii sisi tunazungumza Watalii hawajaweza kufika hata milioni 2,
lakini nchi kama Morocco inapokea Watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka
kwa hiyo ni vyema kushirikana nao katika masuala ya Sekta ya Utalii”,
alisema Rais Magufuli.
Sekta ya Utalii ni chachu kwa
maendeleo ya Taifa kwani inalipatia pato kubwa na kuweza kuimarika
kiuchumi kupitia fedha za kigeni, lakini kwa Tanzania kumekuwa na
upungufu wa ndege kwa kuliona hilo Serikali ya Awamu ya Tano imeweza
kununua ndege kubwa aina ya Boen 787-8 dreamliner ambayo itakuwa inatoka
moja kwa moja kutoka Ulaya, Amerika na kwingineko duniani na kutua
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam.
“Tunataka Watalii wawe wanatoka
Marekani wanakuja moja kwa moja Dar es Salaam, ile ndege inauwezo wa
kutoka Marekani, Australia bila kutua popote”, alisema Rais Magufuli.
Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kuendeleza Utalii kwa kuingia makubaliano na nchi
mbalimbali ikiwemo Serikali Morocco kupitia ziara ya Mfalme Mohammed VI
,ya mwaka 2015 ambapo waliingia makubaliano ya mkataba kwa Sekta ya
Utalii unaolenga kubadilishana Watalii kwani nchi ya Morocco ina idadi
kubwa iliyofikia milioni 12 kwa mwaka 2015 na idadi hiyo inatarajia
kuongezeka mpaka milioni 14 mwaka 2017 kwa hiyo ni vyema kuwa na
ushirikaiano ili kukuza Sekta hii nchini.
- Mradi mkubwa wa umeme (Kinyerezi I na II).
Juhudi kubwa za Serikali ya Awamu
ya Tano yenye malengo makubwa katika kuijenga Tanzania kuwa nchi ya
viwanda imetambua kuwepo kwa viwanda kunaambatana na nishati ya uhakika
ya umeme kwa hiyo Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameweza kuanzisha mradi
mkubwa wa umeme ili kuendana na Sera yake ya Tanzania ya viwanda.
“Umeme ni maendeleo, umeme ni
kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi kwa Taifa lolote duniani, bila ya
kuwepo kwa umeme wa uhakika ndoto yetu ya kujenga uchumi wa viwanda
haitaweza kutimia”, Rais Magufuli.
Katika mradi huu wa umeme ulianza
na kinyerezi I ambayo itaweza kutoa megawati 150 lakini katika uzinduzi
wa ujenzi wa kinyerezi II ambayo itatoa megawati 240 kwa watanzania,
Mradi huu wa kinyerezi II ambao unafadhliwa na Serikali ya Japan
iliyotoa dola za kimarekani milioni 292 ambayo ni asilimia 85 ya ujenzi
huku Tanzania ikitoa dola milioni 120 ambayo ni sawa na asilimia 15 ya
mradi, Uzinduzi huu uliambatana na ongezeko la megawati kinyerezi I
ambapo megawati 180 zitakazogharimu dola milioni 20 jumla ya megawati
330 zitapatikana katika Mradi huo na hii ni faida kubwa kwa Watanzania
wote kwani wataweza kuanzisha viwanda vidovidogo na hatimaye kukuza
uchumi.
“Tunataka tuwe kama nchi zingine
duniani kwa matumizi ya umeme sisi bado tuko wati 30 kwa kila mtuamiaji
wa nishati hii, lakini Kenya wati 40, China wati 490, Afrika ya Kusini
wati 500 na Marekani wati 1,683 kwa kila mtu kwa hiyo sisi bado tuko
nyuma”, Rais Magufuli
Katika mradi huu ambao utajengwa kwa awamu yaani kinyerezi I mpaka VI utasaidia kuondokana na adha ya umeme nchni.
Kwa uchache hayo ndio baadhi ya
mafanikio ambayo JPM ameweza kuyafikia katika kipindi kifupi alichokaa
madarakani, hii ni ishara kuwa hadi atakapomaliza muhula wake Tanzania
itakuwa imepaa kiuchumi na kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Post A Comment: