Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya kukamatwa kwa kamati ya Ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Bariadi baada ya kutafuna mil 4.8. |
Vyoo vya awali vya shule ya msingi Bariadi. |
Mkuu wa shule ya Msingi Bariadi Mayila Ndalahwa akihojiwa na
waandishi wa habari juu ya sakata la vyoo na kahitaji kwa wananfunzi wa
shule hiyo.
Picha zote na COSTANTINE MATHIAS.
NA COSTANTINE MATHIAS, BARIADI.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mkoani
Simiyu, Festo Kiswaga ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kuwakamata na
kuwaweka rumande watu watano ambao ni Kamati ya Ujenzi ya Shule ya Msingi
Bariadi, baada ya kudaiwa kutumia vibaya fedha za ujenzi wa matundu 14 ya vyoo
vya shule hiyo zilizotokana na michango ya wananchi.
Kamati
hiyo inadaiwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 4.8 ambazo zilichangwa na
wananchi kwa ajili ya ujenzi huo ili kupunguza uhaba wa matundu ya vyoo
uliokuwa unaikabili shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1373.
Kiswaga aliwataja waliokamatwa kuwa ni Mlela
Hosea mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, Lucas Gervas Makamu Mwenyekiti, Kenedy
Machume, Wodya Husein na Suzan Ezekiel ambao ni
wajumbe wa kamati hiyo.
Kiswaga aliwaonya wote wenye tabia ya kugusa
fedha zinatokana na michango ya wananchi kuwa serikali yake itawashughulikia
ipasavyo kwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, na kuwataka wananchi
waendelee kuchangia fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Akizungumzia
suala hiyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bariadi Mayila Ndalahwa anasema dalili
za wajumbe hao kufuja fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa
vyoo zilianza kuonekana mapema baada ya kumfukuza fundi aliyekuwa ameidhinishwa
na mkutano mkuu wa wazazi.
‘’kila mzazi alichangia 7600 ili kufanikisha
ujenzi huo, na kamati hiyo ilitokana na wazazi wenyewe…ilionekana walianza
kununua vifaa hewa kwa sababu walikuwa wakichukua fedha nyingi lakini wanaleta
vifaa vichache, mfano saruji’’ alisema Ndalahwa.
Wanafunzi wa darasa la sita Anastazia Pius na
Emanuel Amos walisema wamekuwa wakikutana na foleni kubwa chooni kutokana na
msongamano mkubwa wa wanafunzi sabau ya upungufu wa vyoo kwa sababu wanafunzi
ni wengi tofauti na mahitaji ya vyoo.
Mmoja wa wazazi aliyekuwa Shuleni hapo Mathias
Sakagoi alisema kuwa walichangia ujenzi huo tangu mwezi February lakini hadi
sasa umesimama bila taarifa na hali iliyoawasababisha kutohudhuria vikao vya
shule baada ya kubaini ubadhirifu uliokuwa ukifanyika.
Shule ya msingi Bariadi ina jumla ya wanafunzi
1373, ina matundu 12, na upungufu wa matundu 57 kwa sasa inakabiliwa na tatizo
la uhaba wa matundu ya vyoo kwa muda mrefu ambapo wazazi waliamua kuchangia
ujenzi huo ili kuwanusuru wanafunzi hao.
Post A Comment: