Shughuli za ukarabati wa Bomba hilo zikiendelea. |
Mafundi wakiendelea na shughuli za ukarabati wa Bomba hilo. |
Madiwani 6
wanashikiliwa na Polisi mkoani Geita baada ya kufanya maandamano kinyume cha
sheria na kusababisha uharibifu wa Bomba la Maji la kutoka Nungwe kwenda kwenye
Mgodi wa Dhahau wa GGM.
Kamanda wa
Polisi mkoani Geita Bw Mponjoli Mwabulambo amesema walichofanya madiwani hao
jana hakikubaliki kisheria na kwamba hawakufuata utaratibu wa kufanya maandaman
yao na kwamba wanaendelea na msako wa kuwabahini wale wote ambao wamefanya
kitendo cha kuandamana na kusababisha baadhi ya kazi kusimama siku ya jana.
Amesema
miongoni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja na
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM
wilaya ya Geita kwa tuhuma za kushiriki maandamano na kufanya uharibifu
huo.
“Kwa mtu wa
kawaida sidhani kama alipendezwa na kitendo hicho tuache habari ya kuremba na
kupepesa macho lile tukio sidhani kama ni kitendo kizuri, ni kosa ambalo
walilitenda na kwamba tunawashikilia madiwani sita akiwemo katibu wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita na hicho hakikuwa kizuri lakini
pia kukimbia kwao niseme sio suluhisho tutawakamata”Alisema Mponjoli.
Meneja
Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii kwenye mgodi wa GGM Bw Manase Ndoloma amesema
taarifa za kupasuliwa kwa bomba hilo linalotoa maji safi kutoka ziwa Victoria kupitia kwenye kijiji
cha Nungwe hadi kituo cha usambazaji
maji kwenye Bwawa la Nyakanga walizipata kwa wananchi na ameahidi kuendelea
kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao na kwamba
mgodi haujaathirika kwa kutobolewa kwa bomba hilo.
“Tungependa
kufanya shughuli zetu za kutekeleza miradi ya kuisaidia jamii ya Geita kwa hali
ya usalama lakini pia kwa usalama wa wafanyakazi wetu mgodi wa dhahabu wa Geita
utaendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania pamoja na jamii inayozunguka eneo la mgodi ili kuharakisha urejeshaji
wa maji pamoja na amani kwa ujumla ndani ya mji wa Geita”Alisema Manase.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nungwe Bw Revocatus Masatu
amesema aliwaona watu kutoka halmashauri na magari ya serikali na hakuwa na
taarifa yoyote kuhusu kupasuliwa kwa bomba hilo kwani alijua ni taratibu kwa
halmashauri kutembelea vijiji vyake.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE .
Post A Comment: