MAUJAJI WALIOSHINDWA KWENDA HIJJA KURUDISHIWA PESA ZAO

Share it:
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally amesema pesa za mahujaji wote walioshindwa kwenda katika ibada ya Hijja zitarejeshwa ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.

Sheikh Zubeiry ameyasema hayo katika Baraza la Eid Al Adh’ha na kuwa amefanya uamuzi huo baada ya baadhi ya mahujaji kushindwa kwenda Hijja kutokana na taasisi zilizoandaa safari yao kushindwa kumamilisha taratibu zote zinazohitajika.

Sheikh Zubeiry amesema ataunda kamati maalumu ambayo itakuwa ikizifuatilia taasisi ambazo zinahusika na kusafirisha mahujaji kwenda katika ibada ya Hijja ambayo inafanyika katika mji wa Makkah na Madina.

“Nimekutana na wawakilishi wa taasisi hizo mara mbili na tumekubaliana kuwa pesa hizo zitarusishwa na zitatumika kufanya maandalizi kwa Hijja nyingine labda hii haikuwa bahati yao lakini Hijja ijayo watakwenda,” alisema Sheikh Zubeiry.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika Baraza la Eid,Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi aliwataka Watanzania kudumisha amani iliyopo nchini na kuishi kwa upendo bila kubaguana kwa itikadi za kidini au kikabila.
Share it:

habari

Post A Comment: