|
Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi
na Mauzo wa NMB Omar Mtiga Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. |
|
Baadhi ya walimu ambao wanatoka kwenye halmashauri zilizopo Mkoani Geita wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi
na Mauzo wa NMB Omar Mtiga. |
|
Meneja wa Benki ya NMB Mkoani Geita Mathias Nkuliwa akizungumza wenye Kongamano hilo ambapo alisema lengo la kungamano hilo ni kutambua mchango wa walimu katika Benki ya NMB. |
|
Meneja wa NMB Kanda ya ziwa Abraham Augustino akizungumza na walimu wakati wa Kongamano. |
|
Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita wakimsikiliza meneja wa kanda wakati alipokuwa akizungumza. |
|
Mkuu
wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi
na Mauzo wa NMB Omar Mtiga Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano
ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. |
|
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB wakisikiliza maelezo ya Mkuu
wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi
na Mauzo wa NMB Omar Mtiga wakati akizungumza kwenye Kongamano hilo.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akifungua Kongamano la walimu na Benki ya NMB ambalo limefanyika kwa mala ya kwanza Mkoani Geita. |
|
Baadhi ya wadau wa idara ya Elimu Mkoani Geita wakimtegea sikio Mgeni Rasmi. wakati alipokuwa akizungumza na walimu pamoja na wafanyakazi wa NMB Mkoani Geita. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa Elimu wa Wilaya mbali mbali zilizopo Mkoani Geita. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiondoka na kuagana na Wafanyakazi wa NMB baada ya kuwa amefungua Kongamano hilo. | | | | |
PICHA NA JOEL MADUKA
Imebainika
kuwa bado kuna idadi kubwa ya watanzania wasiotumia mifumo rasmi ya kifedha na
kibenk , ambapo tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia ishirini (20) ndio
wanaotumia huduma za kibenk
huku sababu kubwa ya kutokutumia
ni ukosefu wa elimu na ufahamu wa kutosha kuhusu huduma za Kibenk.
Akizungumza na Walimu ambao walikuwa kwenye kongamano la
siku ya walimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
amesema kuwa ipo sababu ya kuvishawishi vyombo vya kifedha na taasisi nyingine
husika kuwa na program maalumu za kutoa Elimu ya masuala ya kifedha hususani
maeneo ya vijijini.
“Hivyo basi
kuna kila sababu ya kuvishauri vyombo vya fedha na taasisi nyingine husika kuwa
na program maalumu za kutoa elimu ya masuala ya kifedha hususani maeneo ya
vijijini ili watanzania walio wengi zaidi waweze kunufaika na maendeleo
yaliyofikiwa na sekta ya fedha hapa nchini”Alisema Kyunga.
Aidha kwa
upande wake Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB
Omar Mtiga amesema kuwa idadi ya watanzania karibia milioni 50 ni asilimia 20 tu ndio wenye akaunti za benki
, na zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wanamiliki simu za mkononi na wana uwezo
wa kufanya malipo na miamala kupitia simu za mkononi.
“NMB kwa
sasa inaamini katika kutoa huduma za kibenki za kidigitali kwa watanzania wote
,njia hii tunaiona ni bora zaidi na inaendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia
na itasaidia kuleta mwamko mkubwa zaidi kwa watanzania wengi kuweza kutumia
huduma za kibenki kwa kufanya miamala na malipo mbali mbali”Alisema Mtinga .
Mtinga
ameendelea kuelezea kuwa wateja walionao
ni zaidi ya milioni 2.5 kati yao zaidi ya wateja milioni 2 wanatumia simu za
mkononi kufanya miamala na kuangalia salio ,kufanya malipo mbalimbali kama
kulipia umeme hata kulipia kodi mbalimbali.
Aidha kwa
upande wake Mwalimu Imani Amisi ameelezea kuwepo kwa changamoto kubwa ya
kimikopo hususani katika taasisi za Kifedha
kuwepo kwa riba kubwa hali ambayo inasababisha wengi wao kushindwa
kukopa fedha hizo lakini kutokana na maelekezo ambayo wamepatiwa na NMB
wanaamini kuwa Benki hiyo itakuwa mkombozi katika maswala ya Mikopo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Post A Comment: