RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI ALIPATIA JESHI LA POLISI TANZANIA MILIONI 260 ILI KUJENGA NYUMBA ZA POLISI ZILIZOUNGUA JIJINI ARUSHA

Share it:
index
Na Mahmoud Ahmad Arusha  
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amelipatia jeshi la Polisi Tanzania Milioni 260  kutokana na ajali ya moto iliyotokea kwenye makazi ya polisi Arusha September 27 Mwaka huu majira ya saa moja na Nusu usiku.

Akizungumza na Waandishi ya Habari jana Inspecta Jenerali wa polisi Tanzania  IGP Simon Sirro ,alisema kuwa Rais Magufuli ametoa fedha hizo kutokana ya ajali ya moto iliyotokea jana na kusababisha  familia za askari wa polisi 14 na zenye wakazi 44 kupoteza mali na makazi ya kuishi.

Sirro alisema kuwa Jeshi polisi Tanza limetoa kiasi cha shilingi milioni 40 kutoka kwenye mfuko wa Jeshi hilo ili kusaidia kujenga makazi mapya ndani ya mwezi Mmoja na kuzipatia milioni moja kila familia ya askari hao ili kuweza kujikimu kimaisha.

“Rais ameagiza wakala wa Taifa wa majengo { TBA} kuwapatia askari makazi mpaka hapo ujenzi utakapokamilika ndipo waweze kurejea kwenye makazi yao ya kudumu” alisema Sirro.

IGP Sirro amewasisitiza Askari polisi kuwa ajali hiyo iliyotokea ni kama ajali zingingene hivyo waendelee kuwa na imani na serikali wakati wanashughulikia jambo hilo kukamilika mapema ndani ya Mwezi mmoja.
Aidha kamanda Sirro amewaomba Raia wema na Taasisi za Watu Binafsi kujitokeza kutoa msaada kwa wahanga wa tukio la kuunguliwa na nyumba zao na kupoteza mali zao zenye thamani kubwa.
Share it:

habari

Post A Comment: