WANAFUNZI WALIOPATA AJALI YA KUZAMA KWENYE MAJI WILAYA YA GEITA WAKABIDHIWA MTUMBWI WA INJILI KWAAJILI YA KWENDA SHULE

Share it:
Mtumbwi wa Injini  ambao umekabidhiwa kwenye visiwa vya Butwa na Rulegea kwaajili ya kusafirisha wanafunzi ukielekea kwenye makabidhiano.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo wa chama Tawala cha CCM pamoja na wanafunzi Akizungumza kwenye shule ya Msingi ya Butwa wakati wa makabidhiano.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ,Mhandisi Modest Aporinali Akielezea Juu ya ushirikiano ambao wanao kati ya Halmashauri hizo.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,Wilaya ya Geita Barnnabas Mapande akielezea juu ya ilani ya chama hicho katika kutekeleza ahadi ambazo wanatoa kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Geita,Ali Kidwaka akisoma taarifa ya  utekelezaji wa ahadi ambayo wameitoa kwenye vijiji hivyo.




Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikabidhi Mtumbwi huo wa kisasa kwa mwenyekiti wa Rulegea na Butwa.




Serikali Mkoani Geita imekabidhi Mtumbwi wa Injini kwenye Kisiwa cha Rulegea Kijiji cha Butwa, mtumbwi wenye thamani ya Sh Milioni 7 kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi wanaolazimika kuvuka maji kwenda shuleni.

Mtumbwi huo wa kisasa umekabidhiwa kutokana na tukio la kuzama kwa wanafunzi waliokuwa wakitoka shuleni June 22 mwaka huu na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu.

Akikabidhi mtumbwi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezekiel Kyunga, Mkuu wa wilaya ya Geita Bw Herman Kapufi amemtaka mwenyekiti wa kijiji Butwa Bw Mashauri James na wananchi kuweka mchango wa mafuta ya mtumbwi huo.

“Nakukabidhi Mtumbwi huu na vifaa vyake vyote ni jukumu lenu kuutunza na kuhakikisha watoto wanakwenda shule kila siku na isije kutokea mtoto kutokwenda shule naamini kwamba mtautunza na utawafaa zaidi wanafunzi”Alisisitiza Kapufi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw Ali Kidwaka amesema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanikisha upatikanaji wa usafiri huo.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi  mwenyekiti wa kijiji Butwa Bw Mashauri James amemwakikishia Mkuu wa Wilaya kuutunza vizuri mtumbwi huo na kwamba wataweka utaratibu  upatikanaji wa mafuta.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Share it:

habari

Post A Comment: