Wajumbe wa Halmashauri ya chama cha mapinduzi wilaya ya Geita wakiwa kwenye kikao, |
Katibu wa siasa na uenezi Wilaya ya Geita Bw Jonathan Masele Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Geita,Barnabas Mhoja Mapande akielezea juu ya wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais. |
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakichangia Hoja mbali mbali. |
Katibu wa chama cha Mapinduzi(CCM)Wilayani Geita, Julius Peter Akielezea namna ambavyo watanzania watanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa Bidii ikiwa ni pamoja na kulipenda Taifa. |
Chama cha Mapinduzi wilayani Geita kimempongeza Rais Dr John
Magufuli kwa jitihada zake za kusimamia Rasilimali za taifa yakiwemo madini
nchini.
Akizungumza kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama hicho,
Katibu wa siasa na uenezi Bw Jonathan Masele alisema hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Rais
Magufuli zitasaidia maendeleo ya nchi na Taifa litanufaika na Rasilimali
zilizokuwa zikipelekwa nje ya nchi bila utaratibu.
“Tunatambua kuwa juhudi ambazo anazifanya Rais sio za
kubezwa na watanzania kwani tunajua kuwa haya ambayo yanafanywa ni manufaa ya
wote na sio ya chama furani jambo la msingi tuzidi kumuombea Rais wetu kwani
hata yeye anasema tumuombe kwa Mungu”Alisema Masele.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande
ameitaka migodi mingine kujitathimini kupitia kampuni ya Barrick na kuwa
waaminifu kwenye kulipa fedha zinazoendana na shughuli wanazozifanya.
Katibu wa CCM wilaya ya Geita Bw Julius Peter amesema hisa
ambazo zimetolewa na Barrick pamoja na Sh Milioni 700 zilizoafikiwa zitasaidia
kuboresha Miundombinu na kuwanufaisha Watanzania wengi
Post A Comment: