Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na wadau
wengine wa elimu wakijionea hali halisi ya darasa wanalosomea wanafunzi
(Ni tukio la miezi 7 nyuma)
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akikagua jengo la
darasa lililotelekezwa tangu 2013 lililokuwa likijengwa kwa nguvu za
wananchi na kuchukua hatua ya kulimalizia kwa kutumia fedha zake binafsi
(Ni tukio la miezi 7 nyuma).
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akielekea
kuangalia jengo la darasa alilolifadhili kwa kutumia fedha zake binafsi
ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya kujifunzia baada ya kutembelea
shule hiyo ya msingi Kanembwa miezi saba nyuma na kukuta baadhi ya
wanafunzi wakisomea kwenye jengo ambalo ni hatarishi na kuamua
kulimalizia jengo jingine lililokuwa limeterekezwa tangu 2013 lililokuwa
likijengwa kwa nguvu za wananchi.
Muonekano wa Jengo hilo Hivi sasa baada ya Ufadhi wa Mhe. Doto Mashaka Biteko (Mb).
Post A Comment: