MILA POTOFU ZACHANGIA WANAWAKE KUBAGULIWA KWENYE SHUGHULI ZA MADINI.

Share it:
Mtafiti mkuu wa mradi wa BHRT , Wakili Bw,Clarence Kipobota,akiwakilisha taarifa ya awali ya utafiti ya ujumuishwaji wa masuala ya jinsia katika sekta ya madini Mkoani Geita.

Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya madini Mkoani Geita.

Mtafiti mkuu wa mradi wa BHRT , Wakili  Bw,Clarence Kipobota,akielezea vitendo vya mira potofu ambavyo vimekuwa vikiwakandamiza wanawake kwenye maeneo ya machimbo ya dhahabu.

Afisa Mradi wa BHRT Theresia Sawaya akizungumzia shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na shirika hilo.


Wadau wa Taasisi mbali mbali wakifuatilia maelezo ya afisa Mradi wa BHRT.
PICHA NA JOEL MADUKA 



Utafiti  uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la biashara na haki za binadamu  (BHRT) limebaini kwenye sekta ya madini bado kuna mila  potofu  zinazomkandamiza mwanamke  kushiriki kwenye  sekta ya madini kutokna na kwamba mwanamke akishiriki kwenye uchimbaji wa madini akiwa kwenye mzunguko wake wa mwezi ni mkosi na anaweza kusababisha madini kutopatikana pindi anapokuwa kwenye kipindi hicho.

Akizungumza kwenye Mkutano ambao umewakutanisha wananchi wa Mkoani Geita na baadhi ya taasisi ,Mtafiti mkuu wa mradi wa BHRT , Wakili bw Clarence Kipobota,amesema kuwa wakati wanafanya utafiti wamebaini kuwa kundi la wanawake ni watu ambao wamekuwa wakikandamizwa kwa kiasi kikubwa kwenye shughuli za madini kutokana na kuwepo kwa mila potifu na mfumo dume.

“Tumebaini kuwa kuna swala la mila potofu kwamba mwanamke anapokuwa kwenye siku zake haruhusiwi kwenda mlimani kufanya shughuli za uchimbaji kutokana na kwamba anaweza kusababisha madini kutokupatikana”Alisema Kipoboto.

Aidha kwa upande wake Bi,Christina Gamba ameelezea kuwa  wanawake wamekuwa wakipata manyanyaso ya kuzuiliwa kwenda mlimani  kuchimba madini kutokana na kuwepo kwa mila potofu kuwa mwanamke akienda maeneo ya uchimbaji ni Mkosi na mwisho wa siku huishia kufanya shughuli za uchenjuaji.

Katibu Mtendaji wa shirika la maendeleo ya vijana ,Bw Makanya Tumbo amesisitiza kuendelea kuwekwa sawa kwa takwimu za ushirikishwaji wa maswala ya Kijisia .

Afisa Mradi Theresia Sawaya ameelezea lengo la shirikia hilo ni kuendelea kufanya utetezi wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuangalia swala zima la ukiukwaji wa haki za Binadamu ili kuleta utetezi  wa Binadamu.

Share it:

habari

Post A Comment: