Walimu wakiandamana
Walimu wakiandamana.
Mwalimu Emmanuel Magema akieleza kwa nini wameandamana
Mwalimu Theresia Mushi akielezea jinsi tukio lilivyotokea
Wanafunzi wakiwa nje ya madarasa baada ya tukio kutokea
Walimu wakielekea kwenye ofisi ya halmashauri ya mji Kahama
Walimu wakiingia katika ofisi za halmashauri ya Mji Kahama
Walimu wakielekea katika ofisi za halmashauri ya Mji Kahama
Picha kwa Hisani ya Kijukuu Blog
Mwalimu wa Shule ya Sekondari
Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoa wa Shinyanga Grace
Kalinga (39) amefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kujibishana
maneno na Mkuu wa shule hiyo Ismail Ally.
Kwa mujibu wa walimu wa shule hiyo,
tukio hilo limetokea leo Ijumaa Oktoba 13,2017 asubuhi majira ya saa tatu
baada ya mwalimu Grace kwenda kwa mkuu wa shule hiyo kufuatilia ruhusa ya
kwenda masomoni.
Kutokana na tukio hilo walimu hao
wameandamana hadi ofisi ya Afisa Elimu Sekondari ili kushinikiza serikali
imchukulie hatua za kinidhamu mkuu huyo kutokana na kusababisha kifo hicho
ikiwa ni pamoja na kumuundoa katika shule hiyo.
Aidha Walimu hao wamesema mwalimu
huyo amekuwa na tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi jambo ambalo
linawafedhehesha na kwamba asipoondolewa katika shule hiyo basi wao waondolewe
na kupelekwa kwenye shule zingine.
Hata hivyo taarifa zinasema kwamba
walimu hao kwa sasa wanaendelea na mazungumzo na katibu tawala wa wilaya ya Kahama
Timoth Ndanya katika Ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo ili kufikia mwafaka wa suala
hilo.
Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo Ismail
Ally amesema hawezi kulizungumzia hilo kwa sasa kutokana na kuwa katika
harakati za Kupeleka taarifa hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji
wa Kahama.
Mwili wa Marehemu mwalimu Grace
umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mji wa
Kahama huku Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dokta Fredrick Malunde
akithibitisha kupokea mwili huo.
Post A Comment: