Gari mbili aina ya IST yenye thamani ya shilingi milioni 22 yakiwa yamepakiwa nje ya shule hiyo yakisubiliwa kukabidhiwa kwa wanafunzi hao. |
Mwanafunzi ambaye amezwadiwa gari Edina Davis ambaye katika matokeo ya kitaifa alishika nafasi ya Tisa akijaribia gari yake. |
Mgeni Rasmi ambaye yupo katika Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi ,Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila akikata utepe kwaajili ya kuwakabidhi magari wanafunzi hao. |
Mwanafunzi Bihera Kabaruka ambaye alikuwa mshindi wa pili kati ya wanafunzi kumi ambao wamefanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita. |
NA JOEL MADUKA
Mkurugenzi wa Shule binafsi za WAJA zilizopo Mkoani Geita
Mhandisi Chacha Wambura amewazawadia
magari mawili wanafunzi wa kike waliohitumu Kidato cha Sita katika Shule ya
Sekondari ya wasichana WAJA waliotajwa kufanya vizuri katika masomo ya Sayansii
kwenye matokeo ya kidato cha Sita mwaka huu
Akikabidhi Magari hayo mawili aina ya IST yenye thamani ya shilingi milioni 22, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi ,Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila amewataka wanafunzi wengine kuiga mfano wa washindi hao na kuzitaka taasisi nyingine pia kuiga mfano uliooneshwa na Bw.Chacha
Akikabidhi Magari hayo mawili aina ya IST yenye thamani ya shilingi milioni 22, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi ,Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila amewataka wanafunzi wengine kuiga mfano wa washindi hao na kuzitaka taasisi nyingine pia kuiga mfano uliooneshwa na Bw.Chacha
Mmoja wa wanafunzi waliozawadiwa ni Edina
Davis ambaye katika matokeo ya kitaifa alishika nafasi ya Tisa amesema kufanya kwake vizuri na kupatiwa zawadi ya
gari kunatokana na kujituma ili kuipata zawadi ambayo imekuwa ahadi ya
Mkurugenzi wa shule hiyo kwa wanafunzi wote kuwa angewapatia magari washindi
Mwanafunsi
mwingine aliyezawadiwa Gari ni Bihora
Anita Kabayuka ambaye amesema ushindi wake unatokana na kumtegemea Mungu na kwamba zawadi hiyo ni Mwanzo Mzuri .
Post A Comment: