Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akisisitiza Jambo Wakati akitoa salamu
katika kilele Cha Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa
yamefanyika Katika Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Waziri
wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo mbele ya Meneja
uwezeshaji wakulima wadogo katika Benki ya Wakulima Tanzania (TADB) Ndg
Daniel Mabula, Mwingine ni Naibu waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa
Mara Baada ya kutembelea banda la Benki hiyo Wakati wa maadhimisho ya
siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yalifanyika Katika Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi Wakati akitoa salamu
katika kilele Cha Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa
yalifanyika Katika Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto), Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Charles Tizeba na watumishi mbalimbali wa umma wakitembelea mabanda
mbalimbali katika
kilele Cha Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa
yalifanyika Katika Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa amesema kuwa serikali
inatekeleza kwa vitendo kupigaja vita adui njaa, umaskini na maradhi.
Alisema
katika kupiga Vita adui njaa tayari uzalishaji umeongezeka katika mazao
makuu ya chakula hususani mahindi, mchele, mtama, uwele, na mikunde.
Aliyataja
mazao mengine ambayo uzalishaji wake umeongezeka kuwa Ni pamoja na
uzalishaji wa mazao ya jamii ya mizizi kama muhogo, ndizi, viazi vitamu
na mviringo.
Mhe
Dkt Mwanjelwa ameyasema hayo Wakati akitoa salamu katika kilele Cha
Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Katika
Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Alisema
kuongezeka kwa uzalishaji katika mazao hayo kumepelekea Taifa
kujitosheleza kuwa na chakula kwa wastani wa zaidi ya asilimia 100.
Alisema
Mwaka 2016 Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29.1 ya Pato la Taifa
ikilinganishwa na asilimia 29.0 mwaka 2015 ambapo Mchango mkubwa katika
Pato la Taifa ulitokana na Sekta ya Kilimo, ikifuatiwa na Sekta nyingine
za kiuchumi.
Dkt
Mwanjelwa Alisema Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula mwaka huu
isemayo “Badili mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika usalama wa chakula
na maendeleo Vijijini” inaweka umuhimu katika kuweka Mipango na Programu
zinazolenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo
Vijijini; kupunguza utegemezi na kuongeza usawa katika Jamii.
Alisema
Sambamba na hayo pia inaakisi na kutilia msisitizo uhifadhi mazingira
ambayo ndiyo muhimu katika maendeleo ya kilimo na hifadhi ya Jamii ili
kuchochea jitihada za kuondoa umaskini kwa kutumia nguvukazi ya
Rasilimali Watu hususani Vijana ambayo imekuwa ikihamia Mijini kwa
lengo la kujitafutia mahitaji ya muhimu na mazingira bora.
Katika
hatua nyingine Mhe Naibu Waziri alitembelea na kujionea juhudi
zilizofanywa na Wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa Taifa
linajitosheleza kwa chakula, kujipatia bidhaa za viwandani na pia kupata
mazao ya kuuzwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili kumpatia
Mkulima na Mfugaji faida.
Maadhimisho
hayo yalifungwa rasmi jana Octoba 16, 2017 na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt
Charles Tizeba ambapo alisisitiza kuwa mafanikio yanayopatikana katika
sekta ya Kilimo nchini Ni kutokana na juhudi na umahiri na uwajibikaji
unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli yaliyopelekea Nchi kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya
asilimia 100.
Aliupongeza
uongozi wa Mkoa wa Geita kwa maandalizi mazuri na kufanikisha
Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu wa 2017.
Pia
aliwashukuru Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Kilimo kwa ushirikiano
wao kufanilisha Maadhimisho hayo ikiwa Ni pamoja na Shirika la Kimataifa
la Mpango wa Chakula (WFP - World Food Program) sambamba na Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO - Food and Agriculture
Orgization).
Maadhimisho
ya kwanza ya siku ya chakula Duniani yalianza mwaka 1981. Hivyo
maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na
maadhimisho ya miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.
Post A Comment: