![]() | |
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala amemlipua waziri wa zamani
wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya
madaraka na kumlalamikia kupoteza mabilioni ya fedha za Serikali.
Akichangia
Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018, Bungeni Jijini Dodoma,
Dk Kigwangalla ameiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.
Dk
Kigwangala amesema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni
kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini
sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.
Mbali
na tuhuma hiyo, pia alimtuhumu kutumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia
wa kigeni, kipindi cha kampeni zake za kugombea urais 2015, wakati
kampuni ya raia huyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.
Hata
hivyo wakati Kigwangala akitoa tuhuma hizo tayari Nyalandu alishasema
kuwa tuhuma ambazo zimeanza kuibuliwa mitandao dhidi yake si za kweli
bali zinalenga tu kumchafua.
Taarifa hiyo imekuja kipindi ambacho Lazaro Nyalandu amejiondoa CCM na kujiunga CHADEMA.
|
Navigation
Post A Comment: