Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia
msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya
kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na
furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na
mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.
Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu
umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya
kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi.
Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe na siyo
sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika
yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.
Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo:
Magonjwa ya moyo
Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata
magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa
wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo.
Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio
na mengineyo.
Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa
hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo
hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na
maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.
Hivyo ili uweze kuepuka ugonjwa huu unachoptakiwa kufanya ni kuhakisha
unaepuka visababishi vyote vya ugonjwa huu vya msongo, ambavyo
nimekwisha vielezea hapo awali.
Navigation
Post A Comment: