WAHITIMU WA MGAMBO GEITA WAOMBA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWENYE MAKAMPUNI

Share it:
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi  akiongozana na kiongozi Mkuu wa Gwaride pamoja na Mshauri wa majeshi ya akiba Wilayani humo,Luteni Kanali ,Daud Issah Mnyanga wakati walipokuwa wakikagua gwaride.

Mkuu wa wilaya ya Geita  Mwl,Herman Kapufi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani ,Humo akiimba wimbo wa Taifa mala baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.

Baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa zoezi la kufunga mafunzo ya  jeshi la akiba(Mgambo).

 Baadhi ya askari wa jeshi la akiba wakijiandaa kupita mbele ya mgeni rasmi kwaajili ya kutoa heshima.

Moja kati ya viongozi wa Gwaride akiongoza askari wa Mgambo wakati walipokuwa wakitoa heshima kwa mwendo wa taratibu mbele ya mgeni rasmi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita akitazama shughuli na burudani ambazo zilikuwa zikifanyika wakati wa zoezi hilo.


Gwaride likipata kwa mwendo wa taratibu mbele ya mgeni rasmi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita pamoja na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati Gweride lilipokuwa likipita mbele kwaajili ya kutoa heshima.



Makomandoo wa jeshi la akiba wakionesha namna ambavyo wamehiva kwenye suala la kupamba na adui.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ambayo yalikuwa yanafanywa na jeshi la akiba.








Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwk Herman Kapufi akiwatunuku vyeti baadhi ya askari wa mgambo ambao wamehitimu mafunzo.


Mshauri wa jeshi la akiba  wilayani Geita Luteni Kanali ,Daud Issah Mnyanga akimkaribisha mgeni rasmi wakati wa shughuli za kuwaaga askari wa jeshi la akiba.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwahutubia baadhi ya askari ambao wamefudhu mafunzo hayo.
 NA JOEL MADUKA ,GEITA



 Vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba ama Mgambo wilaya Geita, wameiomba serikali kuwapa kipaumbele katika fursa za ajira za ulinzi zinazojitokeza na pia mikataba ya walinzi izingatie maslahi yao.
 
Akisoma Risala kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi, Muhitimu wa mafunzo hayo Helena Nyamtondo alisema ni vyema kwa serikali ikatoa fursa za ajira kwenye Nyanja mbalimbali kwa wahitimu wa mafunzo hayo yakiwemo makampuni binafsi ya ulinzi ambayo yapo wilayani humo.


“Ndugu Mgeni rasmi tunaomba kupitia mafunzo haya sisi kama wahitimu tupate nafasi kwenye makampuni ya ulinzi yakiwemo ya G4S na Mgodini kwakuwa tunaweza kutumia kile ambacho tumefundishwa kuweka usalama kwenye maeneo hayo na swala jingine ni mishahara na mikataba ya walinzi kutokuwa na masirahi hivyo tunaomba kuboreshewa masirahi ya kazi zetu”Alisema Bi,Nyamtondo.


Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alisema  katika kuhakikisha kuwa anashughulikia maombi yao wiki ijayo atakutana na viongozi wa makampuni ya ulinzi kuzungumza nao kuona namna wanavyoweza kuwasaidia wahitimu wa mafunzo hayo kupata ajira kwenye mashirika yao.


Kwa upande wake mshauri wa Mgambo wilayani Geita Luteni Kanali Daud Mnyanga alisemaa katika mafunzo ya mwaka huu wamekutana na changamoto ya vijana kutofika kwa wakati na tatizo la kifedha .


Jumla ya wahitimu 195 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo huku 28 wakishindwa kuhitimu kati ya washiriki 223 walioanza mafunzo hayo awali.
Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

VIONGOZI 11 WA UPINZANI WARUSHIWA KOMBORA LA UFISADI ZITTO KABWE ATAJWA KUWA NI NAMBA MOJA

 Mwanasheria Patrobas Katambi. Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Mae

JOEL MADUKA