WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUANDIKISHWA ILI KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Share it:
Wananchi wa Mtaa wa Yeya wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakiwa wamepanga foleni ili kuandikishwa wapate vitambulisho vya Taifa.

 Mhandi Ichome akisaidia kuwaandikisha wananchi ili waweze kupata vitambulisho vya taifa


 Cosmas Nyasilu Mwenyekiti wa mtaa wa Yeya akiwapigia mhuri fomu za usajili wa vitambulisho vya Taifa wananchi wa mtaa huo iliwaweze kupata vitambulisho vya taifa.

Afisa Habari wa NIDA, Agnes Gerald akikagua moja ya fomu ya mwananchi katika kituo cha kuandikishia vitambulisho vya taifa, Mtaa wa Yeya-Bariadi.

Afisa Usajili wa Nida mkoa wa Simiyu Careen Kuwite akiongea na waandishi wa habari (hawapo Pichani) juu ya zoezi la uandikishaji wananchi katika kata ya Guduwi wilayani Bariadi-Simiyu.


 Albert Rutahiwa aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, katika zoezi la ukaguzi wa uandikishaji wa vitambulisho vya taifa (NIDA), linaloendelea mkoani Simiyu. (picha zote na Costantine Mathias).

NA COSTANTINE MATHIAS, BARIADI.

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imewataka wananchi wa Mkoani Simiyu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho vya taifa katika zoezi la uandikishaji linaloendelea nchi nzima.

Sambamba na hilo, vitambulisho hivyo vitawasaidia wananchi katika kupata huduma mbalimbali muhimu kama mikopo, dhamana na kutobuguziwa wakiwa mipakani.

Akiongea wakati wa ukaguzi wa zoezi hilo katika mtaa wa Yeya mjini Bariadi, Afisa Usajili wa mkoa huo, Careen Kuwite alisema kuwa wanatarajia kuandikisha zaidi ya ya watu 18,000 na zoezi hilo linaendelea vizuri katika wilaya za Bariadi, Busega, Maswa, Itilima na Meatu

Kuwite aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanaandikishwa na kupata vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia katika kuwatambulisha, kupata mikopo na dhamana mahakamani.

Aidha aliwataka wananchi pindi wanapokuja kuandikishwa wabebe viambatanisho ili kurahisisha uandikishaji kama vile vitambulisho vya kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva na vitambulisho vya kazi.

‘’wananchi waandae viambatanisho, wawe na nguo zilizokolea rangi ili kupata picha halisi…pia tumejipanga kukabiliana na hitilafu yeyote juu ya mashine kwa sababu tunao wataalamu wa kutosha’’ alisema Kuwite.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo kiswaga, katibu tawala wa Wilaya hiyo, Albert Rutahiwa alisema kuwa pamoja na zoezi hilo kufanyika kipindi cha msimu wa kilimo wananchi wanatakiwa wajitokeze kwa wingi kwa sababu linafanyika kwa awamu.

Rutahiwa aliwataka wananchi wenye sifa wajitokeze kuandikishwa na wasisite kuwataja wawnanchi ambao watafika kujiandikisha wakati siyo raia wa Tanzania.

Aliwataka watendaji, madiwani na viongozi wengine kuwahamisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili zoezi hilo liweze kufanikiwa.

Kwa upande wake Cosmas Nyasilu Mwenyekiti wa mtaa wa Yeya alisema kuwa baadhi ya wananchi hawajafika kwa wakati kwa sababu maeneno wanayoishi yanazungukwa na mto mpaka maji yapungue.

 
‘’baadhi ya maeneo yanazungukwa na mto, hivyo wananchi wanasuburi maji yapungue ili wafike kujiandikisha, mwitikio wa wananchi ni mzuri, pia wananchi wenyemahitaji maalum kama wazee, wajawazito, wagonjwa na waleamavu tunawapa kipaumbele ili wahudumiwe na kurudi majumbani’’ alisema Nyasilu.

Mmoja wa wananchi aliyekuwa akiandikishwa, Mhandi Mchome alisema kuwa huduma zinatolewa ipasavyo na wananchi wameshatambua umuhimu wa vitambulisho na wamejitokeza kwa wingi.




Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

WANANCHI WA NYAKAGWE WAIOMBA SERIKALI KUWATENGENEZEA DARAJA

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyakagwe wakivuka Mto kwa kuvua viatu kutokana na kukosekana kwa daraja kwenye eneo h

JOEL MADUKA