![]() |
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), BAVICHA wamefanya uteuzi wa viongozi wake ngazi ya Taifa ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kufuatia baadhi ya viongozi wao kukihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.
Katika uteuzi huo, Balaza hilo limemteua aliyekuwa Katibu wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA, baada aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi kuhamia CCM. Ole Sosopo ataitumikia nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani 2018.
Aidha, Bavicha wamemteua Mwalimu John Pambalu kuwa katibu wa Bavicha baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi na Ole Sosopi aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa muda.
Kabla ya maamuzi ya teuzi hizo kufanyika, Baraza la Uongozi la Chama hicho lilikutana jana na kujadiri mwenendo wa chama hicho, kuweka mikakati na malengo yao pamoja na kutoa mwelekeo mpya wa chama. Aidha chamahicho waliojadiri hali ya amani hapa nchini pamoja matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika wiki iliyopita ambapo waliambulia kata moja kati ya 43 zilizofanya uchaguzi na kutoa mapendekezo kwa Bavicha kufanya uteuzi huo.
|
Navigation
Post A Comment: