RC RUVUMA AKANUSHA TAATIFA ZIANAZOZAGAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUWA MAPIGA MARAFUKU KUITA BABY

Share it:
Hii hapa ni video ya hali kile alichokisema wakati akizungumza na wanafunzi wa NASULI SEKONDARI

NA DITHA NYONI
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amepinga marafuku wananchi wa mkoa wa Ruvuma wasiitane baby.
Tamko hilo amelitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ndogo ya mkoa wa Ruvuma , hii inakuja baadaya ya taarifa kuzagaa na yenye picha inayoonesha mavazi tofauti na eneo alilokuwa anatoa ujumbe katika shule ya sekondari NASULI na MBAMBA BAY huku ujumbe ukisomeka “marukuku kuitana baby” mkuu wa  mkoa wa Ruvuma.
Ikumbukwe Novemba 8 mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Ruvuma alifanya ziara katika halimashauri ya natumbo katika shule ya sekondari nasuli na kuzungumza na wanafunzi hao, huku kampeni kubwa ili kuwa ni kueneza ujumbe wa kumtaka mwanafunzi wa kike kuvaa maguni manne ambayo ni sare ya shule,joho la maafari,gauni la harusi,na matreniti dress
“ili muweze kufanikisha masomo yenu watoto wakike lazima mvae magauni ili muweze kufanikisha malengo yenu”pia mkuu wa mkoa wa Ruvuma aliongeza kuwa ni marafuku watoto wa kiume na wakike kuitana baby
“msikubali kuitwa baby kwa sababu kukubali kuitwa baby ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi,mskubali kuitwa queen we ni mwanafunzi unatafuta maisha na wala usikubali kuitwa mrembo au mzuri alisema Rc MNDEME.
Lengo ya kampeni ni kumsaidia mwanafunzi wa kike aweze kufikia ndoto zake za kielimu na kuweza kufanikisha malengo yake.
Kufatia taarifa hizo mkuu wa mkoa alisema ilikuwa inawalenga wanafunzi wa kike na sio watu wazima kwani taarifa zinazoenezwa na makundi ya watu wachache zinalengo la kupotosha umma hivyo wakazi wa mkoa wa Ruvuma wapaswa kupuuzia.
Aidha amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kutumia kauli mbiu hiyo ya magauni manne ili iwe chachu kwa wanafunzi wa kike waweze kufanikisha ndoto zake,kwani wanaofanya hivyo hawana nia nzuri wa watoto wa kike.
Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

BAJAJI WAGOMA KUTOA HUDUMA YA USAFIRI GEITA

Bajaj zikiwa zimepakiwa na waendeshaji mjini Geita baada ya kuwa na madai ya kuonewa na askari. Bw,Joseph Dotto am

JOEL MADUKA