Baadhi ya wajumbe wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi. |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Enock Yakobo akichangia hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)
kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
|
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg
Charles Maganga akiwasilisha taarifa ya Mkoa ya
Maendeleo ya Elimu katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC),
kilchofanyika jana Mjini Bariadi.
|
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista
Wasabato (SDA) Bariadi, Mashauri Bahini akichangia hoja katika Kikao Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) Simiyu
kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
|
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.Seif
Shekalaghe akichangia hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
|
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Wadau wa
Maendeleo Mkoani Simiyu wamekubaliana na Uchangiaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya
shule Mkoani humo hususani vyumba vya madarasa katika shule za Msingi na
Sekondari ili kukabiliana na upungufu uliopo, kutokana na ongezeko la wanafunzi
watakaoanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka 2018.
Makubaliano
hayo yamefikiwa katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa(RCC) kilichofanyika jana Mjini
Bariadi.
Akifungua
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Mkoa huo
unahitaji zaidi ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya
shule hususani Vyumba vya madarasa , hivyo wananchi pamoja na wadau wengine
wanaombwa kuchangia ujenzi huo.
Mtaka
amesema hadi sasa wapo wadau kadhaa walioonesha nia ya kuchangia ujenzi wa
vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na nyumba za walimu kwa kutoa ahadi za
vifaa vya ujenzi vikiwemo saruji na mabati.
Mbunge wa
Jimbo la Bariadi, Mhe.John Chenge amesema suala la Elimu ni si la Serikali Kuu
pekee bali ni pamoja na wananchi, Serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine,
hivyo wananchi wahamasishwe kuchangia ujenzi wa miundombinu hiyo kwa ajili ya maendeleo
ya Elimu mkoani humo.
Akichangia
hoja hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo ameshauri kuwa
hamasa ya ujenzi wa miundombinu ya shule
ifanywe na viongozi wote wa Mkoa, ikiwezekana kwa kubadilishana maeneo ya kwenda
kutoa hamasa ambayo ni tofauti na maeneo wanayofahamika zaidi.
“ Wakati tunaanza ujenzi wa Shule za Kata tulikubaliana
kuwa viongozi tubadilishane uzoefu kwa kila mmoja kwenda kuhamasisha maeneo
ambayo wananchi hawawafahamu na hawajawazoea;
viongozi wa Wilaya ya Bariadi walienda Meatu, wa Meatu wakaenda Maswa,
wa Maswa walienda Bariadi , lile jambo lilifanikiwa sana wananchi walihamasika
wakachangia nashauri tutumie pia mfumo huu tutafanikiwa”alisema.
Kaimu
Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Wanafunzi wanaotarajia
kuingia darasa la kwanza mwaka 2018 ni 109,899 wakati waliomaliza darasa la
saba ni 30,898 hali inayosababisha mahitaji mapya ya vyumba vya madarasa 1757
na madawati 26,334; wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 ni
20,818 waliohitimu kidato cha nne 6195 mahitaji mapya ya vyumba vya madarasa ni
367 na madawati 14,623.
Aidha,
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe.Dkt. Shekalaghe ametoa wito kwa viongozi wenzake
kuwahamasiha wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao ili waweze
kupatiwa chakula cha mchana kwa shule ambazo bado hazijaanza kufanya hivyo,
jambo na ambalo liliungwa mkono na
viongozi wengi
Kuhusu
suala la mimba shuleni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali Mkoani humo itaendelea kuwachukulia hatua
kali za kisheria wale wote watakaobainika kuwapa mimba wanafunzi wa kike.
Mtaka
amesema Serikali Mkoani humo imedhamiria na kuweka mikakati madhubuti ya kuwalinda
watoto wa kike ikiwa ni pamoja na
kujenga mabweni kwa ajili ya wasichana katika shule zote za kata, ili
kuwasaidia kuondokana na vishawishi wanavyoweza kuvipata kutokana na kutembea
mwendo mrefu.
Mtaka pia
alitumia kikao hicho kuwajulisha viongozi na wadau wa Maendeleo Mkoani Simiyu
kuwa Mkoa huo umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania mwaka 2018, hivyo akawataka kujiandaa kwa ajili ya tukio
hilo ambalo litaleta watu zaidi ya 1500 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Post A Comment: