Eneo la soko la Nyawilimelwa ambalo linalalamikiwa na wanakijiji pamoja na wafanyabiashara kutokana na kutokuwa na mpangilio mzuri ndani ya soko hilo. |
Wafanyabiashara kwenye Soko la Nyawilimilwa Kijiji cha
Tinaji wilayani Geita, wameiomba serikali kuwaandalia mazingira ya soko jingine
litakalosaidia kupunguza mlundikano kwenye soko hilo.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwepo kwa soko moja
kijijini hapo kumesababisha mlundikano huku baadhi ya biashara za vyakula na
nafaka zikiwekwa chini jambo linalohatarisha afya za walaji.
Kutokana na hali hiyo, Jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama
cha mapinduzi, UVCCM kata ya Nyawilimilwa imekutana na kujadili mustakabali
tatizo hilo ambapo Mwekiti wa jumuiya
hiyo Hamis Lwezaura amemtaka diwani wa
kata hiyo kuona uwezekano wa kuanza ujenzi wa soko jingine ambalo litaweza
kuwahudumia wananchi wengi zaidi kwenye maeneo hayo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Tinaji Bw Majuto Maliyatabu alisema wanaendelea na
majadiliano kutatua tatizo hilo na kwamba eneo ambalo walikuwa wamepanga
kupeleka soko la samaki limebainika kuwa na mgogoro baina ya wanakijiji na
Serikali hivyo wanaendelea kumsubilia mkuu wa wilaya ya Geita kwaajili ya
kufika kijijini hapo aweze kutatua tatizo lililopo.
Diwani wa kata hiyo Bw Method Mtakulwatila alisema amekwisha wasilisha ombi kwa Halmashauri ya wilaya kuomba ujenzi
wa soko hilo na kwamba kwa sasa wanasubiri fedha zitakazosaidia ujenzi huo
zitoke ndani ya halmashauri .
Post A Comment: