Mgodi wa
dhahabu wa Geita, GGM umekabidhi mradi wa kuwawezesha vijana na wanaweke
kujikwamua kiuchumi wenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 2 kwenye halmashauri
ya mji wa Geita.
Mradi huo
unahusisha shughuli za uchomeleaji wa vyuma, ushonaji wa nguo, utengenezaji wa
viatu na ufyatuaji wa matofali ya kisasa.
Hatua hiyo
imefuatia uamuzi wa serikali mkoani Geita kutaka ikabidhiwe majengo ya mradi
huo yaliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi wa GGM yaliyopo Mtaa wa Magogo
yabadilishwe kuwa Chuo cha Ufundi, VETA kwa lengo la kuwasaidia vijana wengi
zaidi kupata ujuzi wa ufundi Mkoani humo.
Akizungumza
katika makabidhiano ya mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel
amesema atahakikisha taratibu za kuwa chuo zinakamilika kwa muda mfupi huku
akiagiza Halmashauri ya Mji wa Geita kusimamia kikamilifu jambo hilo.
Mmoja wa
wajasiriamali walio katika mradi huo Bw Isack Mabula amesema tangu wawekwe
kwenye mradi huo hawajafanikiwa kujiendeleza kutokana na mgodi kugoma kuendelea
kuwafadhili.
Aidha Mkuu
wa Mkoa wa Geita ametoa onyo kwa wote wanaohujumu miradi ya maendeleo ya
wananchi.
Manase
Ndoroma ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa GGM amesema mategemeo yao ni kuona
mradi huo ukiendelezwa na serikali na kwamba Utawanufaisha wananchi wengi zaidi
hususani vijana na wanawake.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Apolinary amesema mradi huo
utatoa fursa nyingi za kuwawezesha walengwa kujifunza na hatimaye kujitegemea
katika shughuli za kiuchumi.
Post A Comment: