Wananchi
Mkoani Geita Wameiomba Mahakama kutoa mafunzo ya kutosha kuhusu mfumo mpya wa
TEHAMA unaotarajiwa kuanza kutumika kwenye kesi mbalimbali.
Mfumo wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano unatajwa kuwa utaongeza ufanisi kwenye
mahakama kwa maana ya kutoa fursa kwa mwananchi aliye nje ya nchi kutoa
ushahidi kwenye mahakama zilizopo nchini.
“Mfumo
unaweza kuwa ni mzuri lakini tatizo ni elimu ni wananchi wangapi wanaelimu na
mambo ya teknolojia kwanza tukiangalia kuna baadhi yao ni waoga hata kufika
kwenye mahakama leo hii unadhani wataujua mfumo huo mimi naomba mahakama itoe
elimu zaidi na sio kusubilia hadi siku ya Mahakam ndio watoe elimu”Alisema
Kimamba Amiri mkazi wa mjini Geita.
“Kuhusu teknolojia
ambayo inazinduliwa na mahakama itatusaidia kwendana na wakati mimi nafikili
sasa nchi yetu inakwenda na mambo ya teknolojia kitu ninachokiomba kwenye
mahakama ni kuondokana na vitendo vya unyanyasaji kwenye maeneo ya mahakamani”Alisema
John Matiba.
Hata hivyo Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya
Mkoa wa Geita, Ushindi Swalo ambaye alisema
lengo ni kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia karatasi nyingi na kwamba
utaratibu huo utasaidia kuonesha kesi nyingi kwa urahisi zaidi hata kwa mtu
aliyembali kuona kesi yake kama inaendelea kwenye tarehe husika au
imehairishwa.
Aidha mkuu
wa wilaya ya Geita Mwl Herma Kapufi amewataka wananchi kujitahidi kujua sheria
kwa kuwa mambo mengi yanaendeshwa kwa misingi ya sheria.
Post A Comment: