Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa zahanati ya Mwamakiliga.
Serikali
Mkoani Geita imewataka wananchi ambao wameendelea kujitolea kwenye shughuli za
maendeleo hususani ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na shule kuendelea na
juhudi hizo na kwamba Serikali ipo pamoja nao kuunga jitihada hizo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Luhumbi wakati akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Bukuru Kata ya Kafita Wilayani Nyang’hwale kwenye
kampeni aliyoianzisha ya kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati na kituo
cha afya ifikapo Desemba mwaka huu.
Alisema serikali inatambua juhudi zinazoendelea kufanywa na baadhi ya wananchi wenye
mapenzi mema na kwamba serikali hipo nao bega kwa bega kuhakikisha inawasaidia
kutimiza malengo ambayo wamejiwekea kwenye maeneo yao.
Akisoma
taarifa ya uanzishwaji wa zahanati ya Kijiji hicho kwa niaba ya mtendaji Mwl
Timotheo Daniel Njogomi alisema hatua hiyo imekuja baada ya kukosekana kwa
huduma za afya na kuwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma
hizo hali ambayo imeendelea kupelekea waakina mama wajawazito kujifungulia
njiani.
Bw John
Isack ambaye ni diwani wa kata hiyo alisema amekuwa akishirikiana na viongozi
na wananchi wengine katika kujenga zahanati kwenye vijiji vya kata yake ambavyo
bado vinachangamoto kubwa zaidi.
Sanjari na
hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw Hamim Gweyama amewataka watumishi kutumia
vema fedha za miradi zinazopelekwa kwenye maeneo yao.
|
Post A Comment: