Shirika lisilo la
kiserikali Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)
linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI
limemaliza warsha ya siku tatu kwa WAVIU Washauri 46 kutoka
kwenye halmashauri nne za mkoa wa Geita.
WAVIU washauri ni watu
wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru
kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri
wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa wenzao, kujitolea kufuatilia na kufundisha wenzao
kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga
katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.
Akizungumza katika
warsha hiyo, Mratibu wa kuzibiti Ukimwi Mkoani Geita, Dr Joseph Odero
aliwasisitiza WAVIU Washauri kutumia uchache wao kuleta chachu kwenye jamii
ambazo wamekuwa wakishughulika kufanya kazi za ushauri kwa watu ambao wanaishi
na maambukizi ya VVU.
“Mwaka 2017 kwa mkoa wa
Geita asilimia kumi na nne (14%) ya watu walikua wanaishi na maambukizi ya VVU na
themanini na mbili (82%) walikuwa ni wazima sasa tumeona kumbe kwa kutumia dawa
mambo yanawezekana. Lakini pia tumeona wengine wameendelea kwenda kwa waganga
wa jadi hawataki kukubali kwamba wanaishi na VVU hali hii nyie kama WAVIU
washauri mnajukumu la kuhakikisha manawasaidia watu wenye hali hiyo”, alisema Dr. Odero.
Odero ameendelea
kusisitiza uzoefu ambao wameupata kwa siku tatu kutumia vyema mafunzo hayo na
yaonekane kuleta tija kwenye jamii ambazo wanatokea kwani kufanya hivyo
watakuwa wamewasaidia watu ambao wanaishi na maambukizi ya VVU kujiona kuwa
wanathamani kwenye jamii.
Afisa Miradi Huduma
Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe alisema WAVIU
washauri ambao wanahudumiwa na shirika hilo wapo mia moja therathini na sita (136)ambao
shughuli zao ni kutoa ushauri na kuwarudisha wale watu ambao wamekimbia kutumia
dawa za kufubaza makali ya VVU .
Post A Comment: