Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe,Matha Mkupasi akiwapatia Cheti kikundi cha Upendo.
Vijana kumi na mbili(12) kwenye halmashauri ya wilaya ya
Mbongwe Mkoani Geita,wamebuni mbinu ya kuchangishana fedha kwaajili ya kununua pikipiki ambazo
wanatarajia kufanyia shughuli ya ubebaji
wa abiria (Boda doda)kwa lengo la kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Mwenyekiti wa kikundi hicho kinachotambulika kwa jina la Upendo Bw,Bilali Mbaraka amesema kuwa waliamua
kuanzisha utaratibu huo kutokana na kutokupata faida wakati walipokuwa wakikodi
au kuajili kwenye shughuli hiyo ya pikipiki na ndipo walichangishana fedha kwaajili ya kununua
piki piki ambazo zitaweza kuwasaidia kujikwamua kimaisha.
Deus Nashon ni moja kati ya vijana ambao wapo kwenye kikundi
hicho ameelezea kwamba kila mwaka wanamatarajio ya kukusanya kiasi cha shilingi
milioni ishirini na nne kwaajili ya kununua pikipiki zingine ambazo zitawasaidia
kwa vijana waliobakia kwenye kikundi hicho.
Hata hivyo kwa upande wake afisa maendeleo ya vijana wilayani
humo Ismail Mcharo amewataka vijana
ambao awana ajira kubuni mbinu ya kujiunga kwenye vikundi ambavyo vitawasaidia
kuomba mikopo na kujiajiri kwa njia za
ujasiria mali.
Akiwakabidhi pikipiki sita kikundi hicho ,Kiongozi wa mbio za Mwenge
Charles Kabeho amewataka vijana hao kufuata
sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuvaa kofia ngumu pamoja kuwa waaminifu kwenye shughuli zao za usafirishaji wa abiria.
Katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mbongwe mwenge wa uhuru umekimbia umbali wa kilmota 160 na
kuzindua pamoja na kuweka mawe ya msingi
kwenye miradi 10 ambayo imegharimu kiasi cha sh, bilioni 1.1.
|
Post A Comment: