Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea mikakati ya namna ambavyo wananchi hao watakavyo lipwa fidia zao na mgodi wa Nyarugusu. |
Mthaminishaji wa serikali,Bw Bahati Albert akionesha taarifa ya uchunguzi na tathimini ilivyofanyika mbele ya wananchi. |
![]() |
Bwawa la maji ambalo lilimomonyoka na kutililisha maji kwenye mashamba ya wananchi. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Wakazi 50 wa Kitongoji cha Mawemeru Kijiji cha
Ziwani Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita wanatarajiwa kulipwa fidia ya Sh
Milioni 200 kutokana na uharibifu wa mazao yao uliosababishwa na sumu
iliyotiririka kutoka kwenye Bwawa la kuhifadhia maji yenye Kemikali kwenye
mgodi wa Nyarugusu Mine Co.Limited.
Hatua hiyo
imekuja baada ya hivi karibu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Bw Kangi Lugola kuutaka mgodi huo kufanya tathmini kujua
kiasi cha hasara iliyosababishwa na sumu hiyo kasha wananchi walipwe fidia.
Bw Bahati
Albert ambaye ni mthamini wa mazao yaliyoharibika amesema fidia ya kila mmoja
italipwa kutokana na ukubwa wa eneo lake na thamani ya mazao yaliyoharibika
kutokana na sumu na kwamba mwekezaji anatakiwa kulipa jumla ya kiasi cha Sh
milioni mia mbili na mbili na laki saba
na elifu ishirini na tisa.
Mkuu wa
wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewataka wananchi wanaotarajiwa kulipwa
fidia kutambua kuwa fedha hizo zitalipwa kwa utaratibu wa Benki na sio kupewa
mkononi kama wanavyodhani baadhi ya watu.
Mtendaji wa
Kata hiyo Bw Thobias amewashauri wananchi hao kutoyavuna mazao hayo kwa kuwa
yana sumu na kwamba atakayekamatwa atashughulikiwa kisheria.
Mkurugenzi
wa Nyarugusu Mine Co.Limited Bw Fred Masanja amesema kampuni yake inaamini kuwa
mthamini amefanya kazi yake kulingana na kila mmoja kwenye eneo lake na kwamba
tafiti nyingine zitakuja baadaye.
Post A Comment: