Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Bulyanhulu baada ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale. |
Akikabidhi mfano wa hundi hiyo mbele ya madiwani wa halmashauri hiyo Meneja wa Mgodi huo, Benedict Busunzu, alisema kawaida mgodi huo hutoa ushuru kwa Wilaya mbili ya Msalala na Nyangh’hwale kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha alitaja
moja ya miradi mingine
ambayo mgodi huo
umesaidia Wilayani humo
ni pamoja na
mradi wa mkubwa
wa kusambaza maji kwa
wakazi 150,000 wilayani humo,
wenye gharama ya
Shilingi Bilioni 4.5 ambao
unatarajiwa kukamilika mwishoni
mwa mwaka huu.
Aidha kwa
upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Geita, Celestine Gesimba amewataka
madiwani na watendaji wa
halmashauri ya hiyo kuepuka
kutumia fedha zinazotolewa na wadau
mbali mbali kwa ajili ya
miradi ya maendeleo kwa kulipana
posho za vikao,
badala yake zote
zitumike katika miradi kwa
manufaa ya ustawi
wa wakazi wa Wilaya hiyo.
“Ninapenda kuwaonya viongozi
na watendaji ambao mpo hapa Nyangh’wale kuwa
tusitumie hizi fedha kwa
ajili ya kulipana posho
za vikao badala
yake zote zietumike
katika miradi ya
maendeleo kwa jinsi
mtakavyoainisha,”alisema Gesimba.
Aidha Mkurugenzi wa
Wilaya ya hiyo,
Carlos Gwamagobe, pamoja na kushukuru mgodi mgodi
huo kwa kuwapatia fedha
hizo alisema ushuru wa huduma ambayo walikuwa wakipata hapo awali umeshuka kwani kwa kiasi kikubwa kwani walikuwa wakipokea
milioni mia nne kwa miezi sita .
“Tuna imani
kuwa mgodi huu ukianza
shughuli zake kama
ilivyokuwa awali hata
ushuru wa huduma
utaongezeka kwani awali tulikuwa
tukipatiwa kiasi cha
Shilingi Milioni 225
lakini tangu kuibuka
kwa sakata la
Makinikia, ushuru nao
umepungua mara mbili
ya zile za
awali,”alisema Gwamagobe.
Post A Comment: