Barabara ya kutua ndege (run away) yenye urefu wa Mita 300 ambayo kwa sasa hipo kwenye hatua nzuri za mwisho kukamilika. |
Baadhi ya watendaji na wajumbe wa Bodi ya TANAPA wakikagua ujenzi wa mradi wa uwanja wa Ndege Wilayani Chato Mkoani Geita. |
Kukamilika kwa ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wilayani
Chato mkoani Geita unatarajia kuwavutia watalii wengi kutembelea kivutio cha hifadhi ya Taifa cha Rubondo
Kilichopo mkoani humo .
Ujenzi wa uwanja huo umeanza rasmi
mwezi wa Septemba mwaka jana na unatarajia kukamilika Juni mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini (TANAPA), Jenerali Mstaafu George Waitara wakati alipotembelea
uwanja huo pamoja na wajumbe wa bodi hiyo na
baadhi ya watendaji kwa nia ya kujionea maendeleo ya
ujenzi huo ambao umeelezwa kukamilika kwa asilimia 65.
“ Kiukweli niseme kazi kubwa sana ambayo imefanyika ya ujenzi wa uwanja huu utakuwa na faida
kubwa sana kwaajili ya mambo ya utalii na mambo mengine kama ya biashara na
suala jingine kubwa ni kuibua vivutio vingine tupate watalii wengi zaidi , tunatarajia
utakapokamilika utaleta manufaa sana
katika sekta mbali mbali
zikiwemo za utalii
na biashara mkoani
Geita na mikoa
ya jirani,”alisema Waitara.
Kwa
upande wake, Mhandisi
wa ujenzi wa
uwanja huo,Makuye Muhinga,Alisema
uwanja huo wenye barabara
ya kutua ndege (run a way ) yenye urefu wa Mita 300 upo kwenye hatua nzuri
na kwamba wanatarajia kukamilisha mwaka huu ujenzi wa
uwanja.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa huo , Mhandisi Robert Gabriel
Luhumbi ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao wametembelea
uwanja huo alisema kukamilika kwa uwanja huo kutafungua uwigo mpana wa kiuchumi
kutokana na kwamba mkoa utaweza kutembelewa na wageni kutoka mataifa ya nje na
jirani.
“Wito wangu kwa wananchi ni kuhakikisha
wanachangamkia fursa mbalimbali
za maendeleo hasa
uanzishwaji wa viwanda
vidogo vya kuchakata mazao
yalimwayo mkoani humu, na tunaamini uwanja
huu utarahisisha
usafirishaji wa bishara
ambazo watakuwa wanazifanya badala ya kupitia Mwanza sasa hivi wataweza
kupitia kwenye mkoa wao”Alisema Luhumbi.
Jumla ya hifadhi zilizopo nchini ni 16 ambazo
zinatambulika kimataifa ikiwemo na hifadhi ya Rubondo ambayo hipo Mkoani Geita.
Post A Comment: