Mkurugenzi wa halmashauri ya msalala , Simon Berege akizungumza na wananchi baada ya ufunguzi wa maktaba ya shule ya sekondary ya Bulyanhulu.
Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu umezindua na
kukabidhi maktaba iliyogharimu shilingi
milioni 22.6 kwenye shule ya sekondari
Bulyanhulu iliyopo katika halmashauri ya
Msalala wilayani Kahama mkoani wa Shinyanga
kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.
Maktaba hiyo imezinduliwa
na Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Msalala Bw , Simon Berege
na kuhudhuriwa na kaimu Meneja
mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Elias
Kasitila.
Akizungumza wakati uzinduzi huo, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi Bulyanhulu,Elias Kasitila alisema wakati
wakitafakari namna ya kuinua taaluma ya wanafunzi waliona ni vyema wakaimarisha
usomaji wa wanafunzi kwa kuwekeza kwenye
maktaba ambayo itasaidia
kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka kwa jamii inayouzunguka mgodi huo.
Alisema kupitia
mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la
kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea
samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba ambayo itawasaidia wanafunzi na walimu
kwa kiasi kikubwa.
“Misaada inayotolewa na Acacia katika sekta ya elimu ni
sehemu ya sera ya wajibikaji kwa jamii ya kampuni inayojikita katika
kuhakikisha jamii inakuwa endelevu kupitia sekta ya elimu na sera hiyo
inachangia moja kwa moja maono ya taifa hadi kufikia mwaka 2025 na malengo ya
nchi ya kuleta maendeleo endelevu kwa kuhakikisha jamii inapata elimu iliyo
bora”,alisema Kasitila.
Mwakilishi wa shirika la Read International linalojihusisha
na masuala ya elimu,Esther Kalwinzi alisema pesa ambazo zimetolewa na mgodi huo
ni shilingi milioni 22.6 kwa ajili kukarabati darasa kuwa maktaba.
Kwa upande wake,mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa
Halmashauri ya msalala , Simon Berege umeushukuru mgodi
huo pamoja na shirika la Read
International kwa kufadhili maktaba hiyo ya kisasa kwenye shule hiyo na kwamba
itasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujisomea na kujenga uwezo mkubwa kwenye
masomo yao.
Kikubwa zaidi ninacho wasisitiza wanafunzi kuzingatia
masomo na pia wazazi tambueni elimu
ndiyo urithi pekee wa kudumu na wenye kubadilisha maisha ya mtoto kutoka hali
ya chini ya umasikini kuja juu zaidi kimaisha”Alisisitiza Berege.
Hata hivyo mmoja kati ya wanafunzi wa shule hiyo Mussa Rajabu alisema kuzinduliwa kwa maktaba hiyo kutaleta chachu ya kupenda kujisomea zaidi na kwamba
itawasaidia kufanya vizuri kwenye masomo yao.
|
Post A Comment: