Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), Frank Leonard ameiambia Malunde1 blog kuwa mwandishi huyo wa habari amekamatwa na polisi wakati akiwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa leo Alhamis Februari 15,2018.
Amesema wanaendelea kufuatilia sababu za kukamatwa kwake na yupo chini ya ulinzi kwa mahojiano.
"Ni kweli tumepata taarifa za kuwa Nyang'oro amekamatwa kwa mahojiano na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) tunafuatilia kujua zaidi" amesema.
CHANZO/MALUNDE BLOG
Post A Comment: