NA K-VIS BLOG/Khalfan Said,
Mwanza
NAIBU Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony
Mavunde, (pichani juu), ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko
wa Fidia kwa
Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara
moja.
Mhe. Mavunde
ametoa agizo hilo Jumatatu Februari 26, 2018 baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza jijini Mwanza, kubaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la
kisheria kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya
mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi
Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko
huo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter, jiji la Mwanza pekee
lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni
waajiri 482 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku
waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya
Mhe. Naibu Waziri kufanya ziara hiyo ya
ghafla.
Akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, Mhe.
Mavunde pia ameiagiza
WCF kuwafikisha mahakamani mara moja, waajiri wa kampuni ya ujenzi ya
JASCO, (Mkurugenzi Mtendaji Bw.Karan Bachu),
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya Airco
Holdings inayotoa huduma za kusogeza vifurushi na mizigo uwanja
wa ndege wa Mwanza na hoteli ya Belmonte ya jijini humo ambapo
Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo, Bw. Philemon Tei, amejikuta
matatani.
"Naagiza waajiri hao kulipa
michango yote ya nyuma (tangu tarehe 1 Julai 2015 tangu Mfuko ulipoanza
kutekeelza majukumu yake au siku mwajiri aliyoanza kazi zake iwapo ni baada ya
tarehe 1 Julai 2015).
Mhe. Mavunde ameagiza
waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili
kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na
kuchelewesha michango katika Mfuko.
“Ni kosa la
jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza
kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5
jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna
sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.
"Tutatekelza agizo la Mhe. Waziri kama alivyolitoa, na nitoe
rai tu kwa waajiri kote nchini (Tanzania Bara), kutekeleza takwa hilo
la kisheria, kwani hakuna kichaka cha kujificha tutawafikia."
Alisisitiza Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter
katika taarifa yake kwa waandishi wa habari.
NAIBU
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony
Mavunde, (wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Uenmdeshaji (Director of Operations),
Anslem Peter, Afisa Kazi Mfawidi Mkoa wa
Mwanza, Khadija Hersi, wakipitia nyaraka za Hoteli ya Belmonte ya jijini Mwanza
kuona jinsi uongozi wa hoteli hiyo unavyotekeleza Sheria ya Fidia Kwa
wafanyakazi, kwa kujisajili na Mfuko huo. Naibu Waziri alifanya ziara ya
kushtuikiza kwenye kampuni kadhaa jijini Mwanza ambapo hoteli hiyo ilibainika
kutojisajili na aliamuru Mkurugenzi wake kupelekewa mahakamani mara
moja. Wakwanza kulia aliyesimama ni Mkuu wa KItengo cha Mawasiliano na
Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge.
Naibu waziri akiongozana na Bw.
Anslem Peter na afisa mwingine kutoka jijini Mwanza mara baada ya
kukagua ofisi za huduma za vifuriushi na mizigo uwanja wa ndege wa
Mwanza, Airco Holdings.
Mkurugenzi wa Belmonet Hotel ya jijini Mwanza, Bw.Philemon Tei |
Naibu Waziri Mvunde, akizungumza na wafanyakazi wa Airco Holdings ya uwanja wa ndege wa Mwanza. Kushoto ni Bw. Anslem Peter |
Naibu Waziri akiwa kwenye ofisi
za Airco Holdings uwanja wa ndege wa jijini Mwanza
Naibu Waziri akitoa maelekezo
kwa uongozi wa Belmonte Hotel
Maafisa wa WCF, wakiongozwa na
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anslem Peter, (kushoto) na Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, wakitoka
kwenye kiwanda cha kuchakata samaki jijini humo baada ya ukaguzi huo
wa kushtukiza.
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi
ya JASCO, ya jijini Mwanza Bw. Karan Bachu, akijieleza mbele ya Naibu
Waziri Mvunde, (hayupo pichani)
Mhe. Mavunde, (kushoto),
akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa kampuni ya
ujenzi ya JASCO, ya jijini Mwanza Bw. Karan Bachu
Mhe. Mavunde, akizungumza na
wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO ya jijini Mwanza baada ya
kufanya ukaguzi wa kushtukiza leo Februari 26, 2018.
Mhe. Mavunde na maafisa wa WCF
wakiwa ofisi za kampuni ya kuchataka samaki jijini Mwnaza
Mhe. Naibu Waziri akipitia
nayaraka za kampuni ya kuchakata samaki ya jijini Mwnaza wakati wa
ukaguzi wake.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw.
Anslem Peter akimuonyesha nyaraka za kampuni ya uchakataji samaki
jijini Mwanza, ambayo imeanza kuwasilisha michango, lakini bado
haijajisajili na Mfuko, ambapo aliagiza watekeeleze takwa hilo
haraka.
Post A Comment: