Naibu
waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewata wachimbaji wadogo wa mgodi
wa Nyakafulu na Bingwa kudumisha amani na utulivu katika shughuli
zao ikiwemo kujenga desturi ya kufanya usafi wa mazingira
ili kuepukana na magojwa ya mlipuko na iwapo hawatazingatia hayo
migodi hiyo itafungwa.
Hayo aliyasema
wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wachimbaji wadogo kwenye wilaya
za Mbongwe na Geita.
Alisema ni
vyema wachimbaji hao kuzingatia amani na afya zao kwani ndio
utaratibu uliowekwa na serikali iwapo ikitokea magonjwa ya mlipuko
kama kipindupindu migodi hiyo itafungwa mara moja.
“Mpo
hapa kwa sababu ya kauli ya Mheshimiwa Dkt, John Magufuli lakini
vilevile akisikia kwamba hapa hakuna amani na sio wasafi mimi
nitatoa amri ya kufunga mgodi huu kwani wizara yangu ndio
inahusika kutoa leseni hivyo pamoja na hayo yote amani
itawale”alisema Naibu waziri.
Kwa
upande wake Rais wa shirikisho la wachimbaji wadogo wa
madini nchini Bw John Bina aliwasisitiza wachimbaji
wadogo kujenga desturi ya kulipa kodi ili waweze kuchimba kwa
kufata utaratibu, sheria, na kanuni za nchi bila
bugudhi yoyote na wagawane kwa utaratibu bila kudhulumiana kwa
sababu sehemu wanayochimba kuna leseni ya mtu kwa hiyo wachimbe kwa kuweka
akiba ili na wao baadae wakate leseni zao za uchimbaji.
‘’
wachimbaji mmekuwa na tabia ya kula bata na kuhonga pesa zote mnapouza madini
acheni tabia hiyo wekeni akiba mkate leseni zenu za uchimbaji
zitawasaidia hapo baadae”Alisema Bina.
Hata
hivyo wachimbaji hao wamemuomba Naibu waziri wa madini Nyongo
kuwasaidia kupata leseni ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao na vitendea
kazi kwa sababu wamekuwa wakitumia njia za asili katika kufanya shughuli zao za
uchimbaji.
Naibu waziri wa
madini,Staslaus Nyongo amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani Geita,kwa
kutembelea migodi mikubwa na midogo huku akisikiliza kero za wachimbaji wadogo
na kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikiyakabili maeneo hayo.
Post A Comment: