WANACHAMA WATANO WA CCM WAPATA AJALI WAKITOKEA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 41

Share it:

WANACHAMA watano wa CCM mkoani Geita wamepata ajali baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali. 

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi jioni katika eneo la Bwanga wakati walitokea wilayani Bukombe katika maadhimisho ya miaka 41 ya CCM. 

Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika wilayani Bukombe. 

Ambaye ana maumivu sana ni Mwenyekiti wa UWT Sofia Bakari tumewafuata kituo cha Afya Bwanga tuko njiani kumkimbiza hospitalini Geita! 

Rose ana maumivu kwenye kifua anakwenda kwa uchunguzi zaidi lakini hali yake si mbaya sana.pamoja na Katibu wa UWT wilaya ya Geita Happy Nyamasagara. 

Ambao wametoka salama kabisa kwenye ajali hiyo  ni Flora Charles ambaye ni secretary wa CCM wilaya pamoja na mwanaye mwenye umri wa miezi kumi! 

Tuendelee kuwaombea.

Imetolewa na
David Azaria
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Geita!

Share it:

habari

Post A Comment: