Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani.
Na,Joel Maduka ,Chato
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi
shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha
anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na
kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato.
Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa
nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea
kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na
huduma hiyo.
Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi
hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo
ili waweze kuendesha biashara
zao.
Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi
Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo
kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame
na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.
“Nimesikia
kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi
alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi
wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi
siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.
Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini Mkoani
Geita,unatekelezwa na mkandarasi wa Shirika la White City
International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi 16 kwenye
jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani humo na jumla ya fedha ambazo
zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni Sh Bilioni 78.56.
|
Post A Comment: