Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi na baadhi ya viongozi wakati wa shughuli ya uzinduzi wa magereza Wilayani Chato mkoani Geita. |
Na,Joel Maduka,Chato
Waziri wa
Mambo ya ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba amemuagiza mkuu wa jeshi la Polisi
Nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la polisi kufanya
uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Baftaha ambaye
alikuwa ni mwanachuo wa chuo cha usafirishaji (NIT) yaliyotokea wilaya ya
kinondoni jijini Dar es salaam.
Waziri
Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato wakati wa
uzinduzi wa gereza la wilaya ya Chato.
Waziri Dk.
Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua hatua
kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.
"Kama waziri
mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu
ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa
kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahsa katika
maswala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu
zote",Alisema Waziri Mwigulu.
Ameongeza
kusema kuwa amemuelekeza IGP mala baada ya tukio kutokea wafatilie na
wachunguze kubaini wote waliosababisha
tukio la hilo na kuweza kuwafikisha katika mkono sheria ili sheria
ichukue mkondo wake.
Dk. Mwigulu
amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara
kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushilikiano
kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wausika wafikishwe katika vyombo vya
usalama.
Post A Comment: